UNATAKIWA KULA KIASI GANI CHA CHAKULA ILI KUPUNGUA UZITO?

Kupunguza mafuta mwilini kunatokea siyo kwa kubadilisha aina ya vyakula tu bali kupunguza kiasi pia. Watu ambao wapo serious na kutaka kupungua na kuwa fit mara nyingi huhitaji kujua kiasi cha aina gani ya chakula wanatakiwa kula.

Ili kujua kiasi cha chakula ni muhimu kujua kuhusu kipimo cha CALORIES. Calories ni kipimo cha nguvu inayopatikana kwenye chakula. Kama tunavyofahamu chakula kinatupa nguvu, hivyo kila fungu la chakula lina kiasi chake cha nguvu ambayo tunaihitaji.

Kwa siku mwanamke anahitaji calories 2200 wakati mwanaume anahitaji 2500 kutoka mwenye chakula ili kumfanya mwili wake uweze kuendesha shughuli za kawaida kama kutembea, kulala, kupumua nk bila kuongeza mazoezi ya zaidi.

Kila aina ya chakula ina kiasi chake cha calories kwa mfano gramu 1 ya chakula cha wanga na protein zina calories 4 kila moja wakati gramu hiyohiyo moja ya vyakula vya mafuta ina calories 9.

Ina maana ukila wali robo kilo ambayo ni sawa sawa na gramu 250 ni sawa na kuwa umeupa mwili calories 1000 kwa hiyo unabakiwa na 1200 za kuupatia mwili wako katika siku hii.

Unene unatokea pale unapokula zaidi ya kiwango mwili wako unachohitaji. Hivyo kuufanya mwili utunze hii nguvu ya ziada kwa njia ya glycogen na mafuta ambayo aidha yanakuwa ndani au yanaonekana chini ya ngozi kama tumboni mikononi, mgongoni, usoni n.k.

WANGA 1g =4 calories

PROTEIN: 1g = 4 calories

MAFUTA: 1g = 9calories

Ili kupungua uzito ni lazima kula chakula chenye kipimo cha chini ya calories 2200 kwa wanawake.

Kwa mfano ukila calories 1200 kwa siku moja utakuwa umesababisha pungufu ya calories 1000, hivyo ili mwili wako uweze kujimudu uendelee kuishi automatically utatumia chakula kilichohifadhiwa mwilini mwako kwa njia ya mafuta na glycogen ili kufidia calories zilizo pungufu hivyo kusababisha kupungua uzito wa mwili.

Kg 1 ni sawa na kama calories 7000 hivi. Kwa hiyo kwa theory inasemekana ili kupungua Kilo 1 inabidi utengeneze deni la calories 7000 mwilini.

Ina maana ukila calories 1200 kwa siku ndani ya wiki utakuwa umetengeneza deni la calories 7000 hivyo kukufanya upungue karibia na 1 kg.

Hii ni theory tu cha muhimu ukila chini ya kiwango kinachotakiwa utapunguza uzito wa mwili bila kujali ni kiasi gani kwa wiki.

mazoezi ya kukimbia

Mazoezi pia yanaongeza pungufu kwasababu calories 2200 ni kwa ajili ya shughuli za kawaida tu, mazoezi yanaongeza hitaji. Kwa hiyo ukila calories pungufu (mf 1200) na ukafanya mazoezi labda ukatumia(kuburn) calories 200. Basi jumlisha pungufu katika kula =1000 calories + ulizoburn kwa mazoezi 200  calories hivyo jumla ya pungufu inakuwa calories 1200 kwa siku.

Lakini inatokea watu wakawa wanakula kwa pungufu na wasione matokeo sahihi kwenye kupungua uzito. Hii ina sababu mbali mbali moja wapo kuu ikiwa ni kuongezeka uzito wa misuli kutokana na mazoezi.

Ukifanya mazoezi na kula vyakula vya protein kwa kiwango sahihi lazima misuli iongezeke. Hii inasababisha usione tofauti kubwa ya uzito. Ukilinganisha vipimo vya upana wa mwili utaona mabadiliko makubwa sana.

Njia nyingine ni kutumia mzani ambao unapima uzito wa jumla na uzito wa misuli, wa maji na mifupa kivyake vyake. Ukiwa na mzani huu utagundua asilimia ya uzito wa mafuta mwili mwako inapungua wakati ya uzito wa protein inaongezeka.

Wanawake wengi tunaogopa kuongezeka misuli. Ukweli ni kwamba hauwezi kuwa na misuli mikubwa inayoonekana kama wanyanyua vyuma!.

Wale wenyewe wamepitia miaka na miaka ya mazoezi gym na kula vyakula vyenye protein nyingi sana hadi misuli yao kufikia ukubwa ule.

Kwahiyo kuongezeka misuli ni jambo jema na haitaonesha usijali.

Kufahamu na kufuatilia kuhusu calories ni muhimu sana hasa unapoanza jitihada za kupunguza unene ili kufikia malengo. Itakusaidia kuchagua vyakula au vinywaji kwa umakini zaidi na itakujengea tabia ya kusoma ingredients ya vyakula unavyonunua kama soda  na snacks ili kujua kama vinafaa au la.

Wengine wanaweza kuona uvivu/kero kupima chakula na kuhesabu Calories kabla ya kula ila kama upo serious, una malengo na unapenda kupungua kwa muda maalumu jifunze kuanza kuhesabu calories.

Kila kitu kinawezekana kama unakitaka kwa moyo wako wote!

You may also like...

COMMENT