SABABU 5 ZA KUNENEPA TENA BAADA YA KUPUNGUZA UZITO MKUBWA

Moja ya tatizo kubwa ambalo huwakumba watu wengi sana ni kuongezeka uzito baada ya kupunguza uzito mkubwa ndani ya muda fulani.

Kama unasoma makala hii kuna uwezekana hata wewe umewahi kupata janga hili ambalo kwa kweli huumiza sana!

Mara nyingi unaweza kubaki ukipunguza na kuongeza uzito uleule miaka nenda miaka rudi bila kufikia kwenye uzito unaoutamani au ule unaotakiwa kwa afya ya mwili wako.

Ili kuepukana na hili janga ni muhimu kujua kwanini unapunguza uzito na kuongezeka tena wakati mwengine unaongeza na uzito mwengine wa ziada.

1. KUPUNGUZA UZITO MKUBWA NDANI YA MUDA MCHACHE SANA.

Madhara ya kupunguza uzito mkubwa ndani ya muda mchavhe

Asilimia kubwa ya watu wanaofanya diet zinazopunguza uzito haraka sana huongezeka tena uzito tena na zaidi.

Hii ni kwasababu kupunguza uzito ni tabia ya kudumu ambayo inatakiwa ujifunze na kuizoea.

Ukipunguza uzito haraka sana hautapata muda wa kutosha kujifunza ile misingi ya afya ya ulaji na mazoezi ambayo ni muhimu kwa ajili ya kuweza ku maintain uzito salama kwa ajili ya afya yako.

2. KUFATA DIET KALI SANA

Hizi ni zile diet ambazo hauwezi kuzifata kwa muda mrefu sana kwasababu huwa zinalazimu kula chakula kiasi kidogo sana.

Mfano ni diet za juice, za muda mfupi kama diet za wiki moja na zote ambazo zinakulazimu aidha kula aina moja ya chakula au kula chakula kidogo sana.

Baada ya kupunguza uzito mwili wako automatically utaanza kukulazimu kula chakula kingi ili kulipizia virutubisho ulivyokosa wakati unafata aina hizi za diet kwa hiyo kukufanya kurudia uzito wako wa kawaida.

3. KUTUMIA DAWA ZA KUPUNGUZA UZITO

Hii inajieleza yenyewe vizuri kabisa lakini kwa kuelewa zaidi pitia makala hii inayoonesha ukweli kuhusu dawa za kupunguza uzito zinazouzwa na kununuliwa kwa bidii sana!

Ninakuhakikishia kama utatumia dawa za kupunguza uzito kuna uwezekano wa zaidi ya 99.99% kwamba huo uzito uliopunguza utarudi kuanzia siku ya moja hadi mwezi miezi miwili baada ya kumaliza dozi.

Tena miezi miwili ni mingi sana!.

Soma zaidi makala hiyo ya dawa za kupunguza uzito ili uelewe kwanini ninasema hivi.

4. KURUDIA TABIA ZA MWANZO ZA ULAJI.

Ulifanikiwa kupunguza uzito kwasababu ulibadilisha jinsi ulivyokuwa unakula zamani na ukaanza kufata diet fulani .

Baada ya kufikia uzito fulani ulioufurahia lazima utagundua kuwa uliachana kabisa na ule mfumo mzuri mpya wa kula na ukarudia vile vyakula vya mwanzoni.

Kwa mfano wakati wa kupunguza uzito ulikuwa hauli sana ugali, pizza, take away kama chips, burgers, soda, keki nk.

Baada ya kupungua ukaanza tena taratibu ice cream zako, bia, keki, ugali, chapati, vitumbua, chips tena ulivimiss kwa hiyo ndani ya muda mchache unajikuta unarudia kule kule ulikoanza.

5. KUACHA KUFANYA MAZOEZI

Mazoezi ya kupunguza uzito

Mazoezi ni mojawapo ya kitu muhimu katika ku-maintain uzito kwasababu kwanza huyeyusha mafuta au kuchoma calories na pili hujenga misuli ambayo ndiyo kama mashine za kuyeyusha mafuta.

Ni muhimu sana kufanya mazoezi baada ya kupunguza uzito kwasababu utakapoacha kufata diet yako utazidisha kula kwa hiyo mazoezi ndiyo yatasaidia kuchoma zile calories zilizozidi ili zisiende kutunzwa kama mafuta mwilini mwako.

Hizi ndizo sababu kuu zinazosababisha kuongezeka uzito baada ya kupungua.

Ni muhimu kuwa makini ili kutopoteza bidii zote ulizozifanya au utakazoenda kuzifanya katika safari yako na kupunguza uzito na kufikia uzito wa afya.

SOMA HAPA : NJIA 5 ZA KUZUIA KUNENEPA TENA BAADA YA KUPUNGUZA UZITO MKUBWA

Kwenye comments niambie kama umewahi kupunguza uzito mkubwa na kujikuta umeongezeka tena na ulijisikiaje!

You may also like...

1 Response

  1. rebeka daniel says:

    Aisee baada ya kutumia dawa nilipunguza kilo tano ILA baadae ziliongezek mara tatu said cjui nilikuw wap cku zote ckujua kuwa kuna Masomo muhimu hakika dawa za kupunguza uzito sina hamu nazo

COMMENT