NJIA 5 ZA KUZUIA KUNENEPA TENA BAADA YA KUPUNGUZA UZITO MKUBWA

Katika sehemu ya kwanza ya makala hii tumeona sababu zinazopelekea kunenepa baada ya kufanikiwa kupunguza uzito mkubwa tu.

Sehemu hii ya pili ni muhimu kwako kama umewahi kupatwa na tatizo hili na umechoka hivyo upo tayari kupiga hatua ya kudumu.

Pia ni muhimu kama haujaanza safari yako ya kupunguza uzito kwasababu ni vizuri kujifunza jinsi ya ku-maintain uzito pale na wewe utakapofanikiwa kupunguza uzito.

Fata hatua hizi kuzuia kurudia uzito wako wa mwanzo.

1. FANYA MAZOEZI

Mazoezi kupunuza uzito

Unaweza kuacha kufata diet ya kupunguza uzito mara unapofikia malengo yako lakini hautakiwi kuacha kufanya mazoezi kabisa!.

Kufanya mazoezi kutasaidia kuzuia kile chakula unachokula kisibadilishwe kuwa mafuta na kuhifadhiwa mwilini.

Badala yake chakula chote kitatumika kutengeneza nguvu unayotumia kwenye mazoezi.

Mazoezi hasa ya kunyanyua vitu vizito yatakusaidia kuimarisha na kuongeza misuli ambayo ndiyo nyenzo muhimu sana katika kuchoma mafuta hivyo kukuzuia kuongezeka uzito.

Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa watu wanaofanya mazoezi angalau kwa nusu saa kwa siku wanauwezekano mkubwa wa ku-maintain uzito kuliko wale ambao hawafanyi mazoezi. ( 1 , 2 , 3 )

2. ZINGATIA MFUMO SAHIHI WA KULA

Utakapomaliza kufata diet fulani ni muhimu kuendelea kula kwa kuzingatia misingi ya afya badala ya kurudia kula vibaya kama hapo mwanzoni.

Ukirudia kula kila kitu ulichokuwa unakula zamani tena kwa kiasi kile kile kikubwa lazima utapitiwa na uzito uliopoteza utarudi tu.

Endelea kula vyakula vya PROTINI na MBOGA MBOGA kwa wingi pamoja na kunywa maji mengi.

Aina hizi za vyakula zinasaidia sana kuhakikisha unakuwa katika uzito sahihi kwasababu vinashibisha sana hivyo kukufanya usile sana.

Epuka kula kiasi kikubwa cha vyakula vya wanga kama unataka ku-maintain uzito wako.

Unapotaka kula wanga pendelea zaidi kutumia bidhaa za nafaka zisizo kobolewa kama mkate wa brown, tambi za brown, ngano isiyokobolewa au atta pamoja na mchele wa bown.

3. JIPIME UZITO MARA KWA MARA

Kupima  hupunguza na ku-maintain uzito

Ukiwa na tabia ya kujipima uzito angalau kwa wiki moja itakusaidia kuchukua hatua pale utakapojisahau na kuanza kuongezeka uzito tena.

Tafiti zinazonesha kuwa watu wenye tabia ya kujipima uzito huwa wanakula chakula kidogo zaidi kuliko wasiojipima. ( 4 , 5 )

Hii ni kwasababu utakapoona uzito unaongezeka utachukua hatua haraka za kupunguza uzito kwasababu hakuna mtu anayependa aongezeke baada ya kufanya bidii kubwa za kupungua.

4. EPUKANA NA STRESS!

Stress za muda mrefu husababisha kuongezeka kwa homoni ya CORTISOL mwilini.

Hormone hii husababisha kuongezeka uzito kwa kukusababisha kula sana hasa vyakula vyenye sukari nyingi au mafuta.

Ukiwa na stress utajikuta unakula sana ili ujiliwaze kwa kupitia utamu wa chakula kama watu wengine wanavyotumia vilevi kujiliwaza.

Moja wapo ya njia ya kupunguza stress ni kuhakikisha unapata usingizi wa kutosha.

Kukosa usingizi wa kutosha ni mojawapo ya vitu vinavyopelekea hatari ya kuongezeka uzito. ( 6, 7 )

Hii ni kwasababu kukosa usingizi husababisha kuongezeka kwa homoni ya ‘Ghrelin’ ambayo hufahamika kama ‘homoni ya njaa. ( 8 )

Pia watu wasiopata usingizi vizuri huwa na kiasi kidogo cha homoni ya ‘LEPTIN’ ambayo kazi yake ni ku control hamu ya kula. ( 9 )

Kwa hiyo homoni hii ikiwa imepungua utajikuta kuwa unakula mara kwa mara kwasababu hakuna kitu cha kuzuia hamu yako ya kula.

5. TAFUTA SAPOTI

vya mazoezi ya kupunguza unene

Ungana na watu ambao wapo kwenye safari ya kupunguza uzito na kuishi maisha ya afya kwa kufata misingi ya lishe sahihi na mazoezi ya viungo.

Sapoti hii unaweza pata kwa ndugu jamaa na marafiki lakini mara nyingi hupatikana kwenye vikundi vya mazoezi mtaani kwenu, mtandaoni au gym.

Ukiwa na mtu au kundi la watu wenye malengo sawa na yako hautaweza kujisahau sana kwasababu mtakuwa mnashirikishana taarifa za maendeleo na kupeana moyo.

Kama hauna kikundi ni vizuri kuanzisha cha kwako.

Ukifata dondoo hizi basi kuwa na uhakika kuwa hautakuja kupata shida ya kuongezeka uzito kila baada ya kupungua.

Usikate tamaa, kila safari ya mafanikio huwa ina kupanda na kushuka. Cha muhimu ni kuendelea na kuongeza bidii!

You may also like...

COMMENT