NJIA 3 ZA KUPUNGUZA TUMBO HARAKA.
Kuna njia nyingi za kupunguza uzito haraka lakini nyingi huwa zinakulazimisha ukae na njaa siku nzima hadi unajisikia kukata tamaa!. Hii ni njia rahisi zaidi kwa sababu una uwezo wa kula ukashiba na kukifurahia chakula.
Kabla haujaendelea ni muhimu kukumbuka aina hii ya kupunguza unene unayoenda kuisoma haitakiwi uiache baada ya muda mchache.
Ili upate mafanikio ya kudumu zaidi unashauriwa kuifuatilia kwa muda mrefu zaidi.
1. PUNGUZA SUKARI NA VYAKULA VYA WANGA KWA UJUMLA.

Kutokula vyakula vya wanga kunasaidia kupunguza njaa hivyo kunafanya upunguze kiasi cha chakula unachokula. (1)
Kwasababu miili yetu hutumia wanga kutengeneza nguvu ya kujikimu na shughuli zote za mwili, uhaba wa fungu hili la chakula mwilini husababisha miili yetu kutafuta mbadala wa kutengenezea hii nguvu kwa ajili ya uhai.
Kwahiyo miili yetu huamua kutumia glycogen na mafuta ambayo yanakuwa yametunzwa mwilini ambayo yanafanya tuonekane wanene ili kutengeneza nguvu kwa ajili yetu.
Mafuta yanapotumika kutengeneza nguvu badala ya wanga ndipo tutaona mabadiliko ya kupungua mwili.
Pia kupunguza vyakula vya wanga kunaleta kupungua kwa hormone ya insulin. Hii inasababisha figo kuondoa chumvi na maji mwilini hivyo kama tumbo limejaa linapungua haraka sana.(2,3)
Mara nyingi watu wanapata tumbo kujaa(bloating) na wanadhani ni gesi tu inasababisha lakini kula vyakula vingi vya wanga na chumvi nyingi kunasababisha mwili ujae maji hivyo tumbo linakuwa limechomoza sana.
Kwa kifupi kupunguza vyakula vya wanga automatically vinaulazimu mwili uyeyushe mafuta!.
2. KULA PROTINI, MBOGA MBOGA NA MAFUTA YA MIMEA.

Hakikisha kila mlo wako una protein, kuanzia chakula cha asubuhi!. Chai na chapati/maadazi/vitumbua/cutlets/mihogo/viazi/keki/ kipi sijataja hapo? achana navyo kabisa.
Kila mlo lazima uwe na protein na mbogamboga.
Mfano wa vyakula vyenye protini:
- Nyama: Ya ng’ombe, kuku, mbuzi n.k
- Samaki: Salmon, sato, sangara, prawns n.k
- Mayai: Ya kuku wa kienyeji ni mazuri zaidi
- Mbegu na karanga: Mbegu za chia, karanga za almonds
Vyakula vya aina ya protein vinafaida kubwa sana katika kupunguza uzito wa mwili kama tulivyoongelea kwenye makala hii.
Utajisikia kushiba kwa muda mrefu, hamu ya kula kula hovyo au kula usiku wa manane vitapungua sana hivyo kukufanya kula kwa kiasi.
Mboga mboga vyenye wanga kidogo ni kama :
Cabbage
broccoli
Spinach
Mchicha
Cauliflower
lettuce n.k
Usijinyime mboga mboga katika kila mlo kwasababu zina nyuzinyuzi ambazo zinasaidia pia kukufanya ushibe haraka. Pia zina vitamins na madini mengine muhimu zinazohitajika mwilini.
TUMIA MAFUTA YASIYO NA LEHEMU (CHOLESTEROL)

Mfano:
- Mafuta ya alizeti
- Mafuta ya nazi
- Mafuta ya Olive
- Mafuta ya ufuta
- Parachichi
- Karanga: Almonds, hazelnuts n.k
Mafuta yanayotokana na mimea ni mafuta yenye afya hivyo muhimu kutumia katika kila mlo.
3. FANYA MAZOEZI YA KUNYANYUA UZITO
Ukipunguza vyakula vya wanga ni muhimu kutopunguza mafuta aina hii, ukipunguza mafungu haya mawili ya chakula kwa wakati mmoja utapata tabu sana na hautafurahia healthy lifestyle yako.
Pia utajisikia uchovu na kukosa nguvu muda mwingi, kwahiyo usisahau kutumia healthy fats kwenye milo yote.
Siyo lazima ufanye mazoezi kwenye plan hii lakini ukitumia siku 3-4 kufanya mazoezi sanasana ya weight lifting matokeo yatakuwa makubwa zaidi.
Kama hauwezi kunyanyua uzito basi unaweza kufanya mazoezi ya cardio kama jogging,kuendesha baiskeli, kuogelea, zumba nk.
Unaweza kuchagua siku moja tu katika wiki kula vyakula vya wanga kama wali/ugali/viazi/chapati n.k
Utaongezeka uzito kidogo tu ambao unasababishwa na maji kwasababu kula vyakula vya wanga kunafanya mwili ushilikile maji mengi, ukipunguza tena vyakula hivi figo itatoa hayo maji na uo uzito kidogo ulioongezeka utatoka. kwa hiyo
USIOGOPE/USISHTUKE/USISHANGAE! Ni kitu simple tu.
Jitahidi ujicontrol usipitilize siku moja tu ya kula hivi vyakula vya wanga, na pia usifanye maajabu kwa kula hadi kupitiliza kama kulipizia. Ni muhimu kujifunza kujicontrol.
Kula kadri ya mahitaji, usipitilize.
PATA DIET YENYE RATIBA YA CHAKULA YA MIEZI MIWILI UPUNGUZE TUMBO HARAKA!

BONUS TIP:
Kunywa maji mengi ukizingatia kiasi cha maji unachokihitaji kutokana na uzito wa mwili wako. Maji yatakusaidia kutosikia njaa pia yataharakisha figo kutoa water weight hivyo kupunguza muonekano wa tumbo kujaa.
Jaribu Kufuata muongozo huu kwa wiki moja kwanza uone matokeo yake, watu wengi hupunguza uzito wa hadi kilo 4 na kila wiki zinazoendelea wanaendelea kupunguza unene.
Nitafurahi ukitupa feedback ya experience na matokeo yako! All the best!
Hugs, GG.
Asante kwa somo zuri nmeipenda Sana,ubarikiwe
Amen!, Karibu sana my dear, Asante na wewe kwa kusoma!
Hellou dada maenda mimi nahitaji kuondoa nyama uzembe na mikono kuwa minene! nifanyaje?
Hi dear! fata hii link utakuta makala nzuri ya kupunguza mikono! https://gigimaenda.co.tz/mazoezi-3-ya-kupunguza-unene-wa-mikono-haraka/
Asante na wwe kwa somo zuri , pia nikuulize maji ya bilinganya husaidia kupunguza uzito na tumbo ni kweli
Asante sana kwa kusoma!🤗 Maji ya bilinganya sijawahi kuyasikia lakini bilinganya zenyewe ni nzuri kwa kupunguza uzito kwa ujumla kwasababu zina calories chache hiku zikuwa na nyuzi nyuzi (fibre) nyingi, hii inaleta kushiba haraka na kuondoa hamu ya kula sana. Nitatafuta tafiti kuhusu maji ya bilinganya nikipata nitaandikia makala ya maelekezo karibu sanaaa!
Hi!
hongera kwa kazi hii njema sana. A lot to speak on, simpiesty is Hongera sana. Nahitaji hiki kitabu ktk hard copy. is it possible?
Asante sana, comment yako imenipa moyo kwa kiasi ambacho hauwezi kuamini. Kwa sasa ninaweza kuafford kutengeneza soft copy tu, lakini lengo langu KUBWA ni kuweza kupublish na hard copy za vitabu vingi tu ambavyo ninaviandika. Ipo siku nitalitimiza na wewe utakuwa kati ya watu wa kwanza kupata taarifa kwa hiyo tafadhali nivumilie. Asante tena na Uwe na siku njema!
Hello…napataje softcopy ya kitabu
Hi! hii hapa link itakupeleka kwenye ukurasa wa kudownload kitabu. Ukishaweka email address yako utakikuta kwenye inbox tayari kwa kudownload! Asante sanaa!
https://mailchi.mp/6ef45cf4ae42/kitabu-free
naanza leo baada ya wiki mbili ntatoa mrejesho
Jmn nahitaji punguza mwil na tumbo kwa haraka sijui nifanyeje
Inawezekana my dear! Anza leo, kunywa nusu lita ya maji kabla haujaanza kula. Kula vyakula vya protein kwa wingi kama nyama na maharage, na ongeza mbogamboga yaani ikiwezekana nunua fungu lako peke yako la mboga. Vyakula vya wanga kula kula kidogo sana! yaani ugali,wali,viazi, mihogo,chapati,maandazi kaa navyo mbali. Mwisho fanya mazoezi angalau kwa nusu saa kwa siku utaanza kuona tumbo linapungua kwa muda mfupi tu.
Asante dear nimefurahia someone Mimi tumbo ndo kikwazo nataka nipunguze
Asante na wewe kwa kusoma dear. Wala usijali yaani linapungua weka bidii tu na ukazane. Mimi mwenyewe ilikuwa kikwazo lakini nikajakugundua wala sio ngumu kihivyo yaani.! Jitahidi mummy!
Asante Kwa Somo Nzuri
Asante sana na wewe kwa kutembelea na kusoma post hii.
Asante nimepata k
itu chakufanya sasa
Nimefurahi kama umepata kitu!🤗 Karibu tena!💪🏾
Ahsante mtaalam kwa utaalamu wako mzuri ila mimi ni mwanaume na nahitaji kupunguza tumbo na uzito corz nina miaka 24 ila uzito nina 98kg sasa inanisumbua kichwa pls help me nataka kuwa na 75kg tuu nikifanikiwa nitakupa zawadi nzuri, , ,
Karibu sana! Unaweza kufikia huo uzito unaotaka Isaack yaani cha muhimu amua kuanza seriously halafu usikate tamaa njiani. Kisayansi ni rahisi zaidi kwa wanaume kupunguza uzito na kujenga misuli kuliko wanawake. Anza taratibu kwa kupunguza matumizi ya sukari hasa kwenye vinywaji kama soda na juice, halafu punguza vyakula vingine vya wanga kama ugali,wali, chips na vyakula vya ngano. Badala yake ongeza kiasi cha vyakula vya protein kama nyama, samaki, mayai, jamii ya kunde, mtindi na aina mbali mbali za karanga na mbegu kama chia seeds na almonds. Mwisho anza kufanya mazoezi ya cardio na ya uzito angalau dakika 45 – saa 1 kuanzia siku 3-5 kwa wiki na utaona mwili wako ukibadilika! Ukihitaji ushauri zaidi na mpangilio wa chakula tuma ujumbe whatsapp 0714 97 55 04 upate meal plans!
Thanks so much naanza leo
Karibu dear! 🤗 Hongera kwa kuanza leo! Unaweza! Kazana na enjoy chakula na mazoezi pia.
Msaada Naitaji Kupungua Uzito Pamoja Na Tumbo
My name is Ann please help me to loss weight sina Raha na maisha kambisa am 34 weight of 120 please help
Hi Ann!🤗 Oh I understand how you feel! Hata mimi nilianza na 120 kg! Hadi sasa hivi nimepunguza 36 kg na I’m still happily going forward 💃🏾. My point is IT IS POSSIBLE, no need of pills/shortcuts nor wasting a lot of money. It’s all about knowing what to eat and when to eat it👌Just send me your email address to [email protected] au text me through Whatsapp +255 714 97 55 04 so that I can give you some deeper guidelines 🤗. You can definitely do this Ann! 💪🏾
jtatu naanza na mm.tumbo linakera hata ukivaa nguo unachukiza upendezi.
Yaani anza dear 💪🏾 Ukikazana linaisha kabisa hadi utakuwa unaenjoy kuvaa nguo zako!💃🏾🤗
Hi…nashukuru kwa kwel kwa somo mi nimeshaanza mazoez japo nafanya Mara moja kwa siku shida yangu kwenye mpangilio wa mlo kuanzia asubuh ad mda wa kulala naomba msaada wako plz….nakuja watsup nipate angalau mfululizo wa wiki nzima then mwez
Karibu dear nitakutumia sample ya mpangilio wa chakula angalau ya wiki 2 uanze nayo!🤗
Hi thanks for lesson i understand but can yu pls help me to loose weight am 18 i have 70kg arethey enough or
Hello! Thanks for reading! There is a measurement called the BMI which tells you if you have normal weight or are overweight. Click on this link to see how you can calculate and check your results! ( https://gigimaenda.co.tz/jinsi-ya-kujua-kama-una-uzito-uliopitiliza-au-obesity/ ) In order to lose weight you have to decrease the amount of food you eat an increase activities. After you have calculated your BMI send me a text on WhatsApp 0714 97 55 04 ana I’ll send you a free meal plan that will give you an idea on how to eat in order to lose weight! Karibu sana!
Hello, je ni ukweli kwamba broiler wananenepesha?
Hi! Katika suala la kuongezeka uzito tatizo si aina ya kuku, tatizo ni wingi, sehemu au aina ya kipande na aina ya upikaji (Kuchemsha, kuchoma, kuoka au kukanga).
jambo jema sana kufundishana n kupeana mbinu mbalimbali za kutunza afya,be blessed guyz.
Amen! asante sana na wewe kwa kujifunza! Ninaamini na wewe utawaelimisha wengine wanaohitaji kujifunza! Karibu tena!
kwa aliyejifungua kwa operation afanye nini ili kupunguza tumbo?
Bonyeza hii link dear utaweza kupata somo kwa ajili ya wamama waliojifungua!!
https://gigimaenda.co.tz/jinsi-ya-kupunguza-tumbo-baada-ya-kujifungua/
Jamani Asante Sana..kwa kweli Mimi Hadi najichukia hili tumbo tangu nimejifungua nna Mwaka sasa lakin tumbo Kama la mimba ya miezi 6 nisaidie mamy…niondokane na aibu hii
Karibu sana dear, wala usijichukie, ukijiamulia na ukipata diet sahihi lazima upungue tu! Ratiba ya chakula ya diet ipo Whatsapp 0714 975504, karibu sana!
Asante sana ngoja na mimi nianze leo
Karibu sana dear!🤗 Anza kwa kweli! Utafurahi na utafamani ungeanza mapema!
Mm sina uzito mkubwa ila nina tumbo la chini linalonikera mno naweza kupunguza tumbo pasi kupungua mwili?
Habari dear🤗
Kama vile una mafuta tumboni tu na si sehemu nyingine basi yatatoka.
Lakini kama kuna mafuta sehemu nyingine basi mwili wako ndio unaamua wenyewe utoe yapi.
Kama katika maisha yako umewahi kuwa na tumbo dogo na mwili size unayopenda basi unaweza kurudia umbo hilo🤗
Cha muhimu fanya tu diet na mazoezi ili upunguze mafuta, halafu kama utaona umepungua sana sehemu nyingine basi utaanza kuongeza vyakula sahihi hasa protini huku ukifanya mazoezi ya hizo sehemu za mwili unazotaka ziwe kubwa!
Hi dear, mimi nimenenepa baada ya kijifungua sasa hivi ni mezi saba hadi shepu yangu imeharibika sieleweki nyuma wala mbele, nifanyeje jamani maana nanenepa mikono, kifua na tumbo.
Ooh yaani wala usiwaze dear! Wamama wengi wanaanza kama wewe hivi hivi yaani! Na baadaye wanapungua vizuri tu! Cha muhimu ni kuanza na kutokata tamaa!💃🏾💪🏾 Plan nzuri ni kupunguza vyakula vya wanga kidogo tu! Kuongeza mboga za majani na maji ya kunywa! Hakikisha kila unachokula unakiandika, kwasababu watu wengi huwa wanakula sana bila hata kujijua!
bonyeza hii link ( https://gigimaenda.co.tz/jinsi-ya-kupunguza-uzito-kwa-mama-wanaonyonyesha/ ) usome maelekezo zaidi kwa ajili ya wamama wanaonyonyesha my dear🤗 Na Kama unahitaji ratiba ya chakula kwa ajili ya wamama wanaonyonyesha basi ukishamaliza kupitia makala kwenye hiyo link ni text Whatsapp 0714 975504 nikutumie sample🤗
Me nasikiaga tumbo la operation halipunguagi je ni kweli?
Si kweli🤗,wapo wanawake wengi sana wamejifungua kwa operation na wanapungua.
Inkwell juice ya lemon, ginger na asal inasaidia kupunguza tumbo kwa haraka
Hi Melly ! Asante kwa swali zuri. Please Fata hii link utapata maelekezo ya kiundani nimeelekeza vizuri kabisa dear🤗. ( https://gigimaenda.co.tz/kunywa-maji-ya-moto-na-limao-asubuhi-husaidia-kupunguza-uzito/ )