NJIA 3 RAHISI ZA KUKUFANYA UACHE KULA SANA ILI UPUNGUZE UZITO HARAKA

Kula sana ni moja ya vikwazo vikubwa vinavyofanya watu wengi washindwe kufata diet za kupunguza uzito wa mwili.

Hii inaweza kuwa kwasababu ya mfuko wa tumbo kuwa flexible zaidi kutanuka kutokana na miaka na miaka ya kuwa na tabia ya kula chakula kingi sana.

Kama ungependa kuacha tabia ya kula chakula kingi sana ili uanze kupunguza uzito wa mwili wako fuata ushauri ufuatao na utaona mabadiliko makubwa sana!.

1. KUNYWA MAJI MENGI

Kunywa glasi moja kubwa ya maji kabla ya kula husaidia kupunguza kiasi cha chakula unachoweza kula kwasababu inafanya tumbo lijae na hivyo kupunguza hamu ya kula na kukufanya usikie umeshiba haraka.

Kunywa maji mengi kwa siku pia husaidia kukuepusha kula kula bila mpangilio.

2. KULA VYAKULA VYENYE KIASI KIKUBWA CHA NYUZI NYUZI/FIBRE.

vyakula vya kupunguza uzito

Vyakula aina hii mara nyingi hufanya ujisikie umeshiba haraka bila kujaza calories nyingi mwilini. Hii ni kwasababu vyakula vingi vyenye kiasi kikubwa cha nyuzi nyuzi huwa na calories chache na pia huchukua muda mrefu kumeng’enywa tumboni.

Pia aina ya nyuzi nyuzi zinazopatikana kwenye mimea (soluble fibre) husababisha kupunguza hamu ya chakula na hukufanya ujisikie umeshiba kwa njia zilizoelezewa kwa kina kwenye post ya jinsi ya kupunguza mwili bila diet wala mazoezi.

Mfano wa vyakula vyenye kiasi kikubwa cha nyuzi nyuzi:

 • Nafaka zisizokobolewa (Brown rice, brown bread,aatta)
 • Jamii ya kunde (maharage, choroko, njegere nk)
 • Karanga na mbegu (Almonds, korosho,macadamia,hazelnuts,chia seeds, flax seeds, mbegu za maboga, mbegu za alizeti nk)
 • Baadhi ya matunda mf parachichi, machungwa, ndizi mbichi nk
 • Mboga mboga mf mboga za majani, broccoli, cauliflower, zucchini, celery nk
 • Maganda ya matunda kama kiwi, maembe, nyanya, zabibu nk

3. KULA PROTEIN KWA WINGI

diet ya kupunguza uzito haraka

Kama ulivyoona kwenye makala ya jinsi ya kupunguza unene bila diet wala mazoezi yakula vya protein vinasaidia sana kupunguza uzito wa mwili kwa kukuzuia kutokula chakula kingi kupitiliza.

Vyakula vya aina hii huchukua muda mrefu tumboni kumeng’enywa hivyo kukufanya ujisikie umeshiba kwa muda mrefu sana.

Mfano wa vyakula vya protein ni kama

 • Nyama
 • Samaki
 • Mayai
 • Maziwa/mtindi
 • Unga wa protein (Protein powders)
 • Jamii ya kunde mf maharage, njegere,choroko nk
 • Mboga mboga ( Broccoli)
 • Karanga na mbegu (Almonds, hazel nuts, mbegu za chia, mbegu za flax, mbegu za maboga nk)
 • Oats na Quinoa

Kwa kifupi:

Ili kuacha kula chakula sana na kuongezeka uzito wa mwili ni muhimu kula au kunywa vitu vinavyofanya tumbo lako liwe limejaa au lina chakula chenye calories chache kwa muda mrefu mfano maji, vyakula vyenye kiasi kikubwa cha nyuzinyuzi (fibre) na proteins.

punguza uzito haraka

You may also like...

2 Responses

 1. Ritha says:

  Na hivyo vyakula vya protine napikaje na natumiaje wakati wakula.

  • GigiMaenda says:

   Vyakula vya Protini kama nyama, samaki na mayai unaweza kuchemsha, kuoka au kuchoma. Kukaanga hakutakiwi kuzidi kijiko kimoja kikubwa cha chakula kwa hiyo ni vizuri kuchemsha kwanza ndipo kukaanga kwa mbali pale inapohitajika. Protini nyingine kama maharage haunashida ya kuziunga, na mayai unaweza kuchemsha au kukaanga kwa mafuta kijiko kikubwa kimoja kushuka chini!

COMMENT