NI KWELI BIA ZINASABABISHA KITAMBI?

Ni jambo linaloaminiwa na watu wengi dunia nzima kuwa unywaji wa bia ndiyo unaosababisha kuongezeka kwa ukubwa wa tumbo hasa kwa wanaume.

Lakini je kuna ukweli wowote katika madai haya? Bia ina kitu ndani yake ambacho husababisha kuongezeka kwa mafuta tumboni?.

Utapata majibu ya maswali yote haya katika makala hii ambayo itakuwa katika sehemu tatu.

Lakini kabla ya kufahamu jinsi gani bia inasemekana kusababisha kitambi ni muhimu utambue jinsi bia inavyotengenezwa.

MAHITAJI YA UTENGENEZAJI WA BIA

Kuna vitu vinne muhimu sana vinavyotumika kutengeneza bia.

  1. Shayiri (Barley; aina ya nafaka kama ngano, mchele, uwele, ulezi nk)
  2. Maji
  3. Mihopi (Hops; aina ya maua yanayoipa bia ladha ya uchachu)
  4. Amira

HATUA 4 ZA KUTENGENEZA BIA

1 KUTENGENEZA KIMEA

MUDA: Uoteshaji siku 5-7

Kiasi maalumu cha shayiri iliyotolewa uchafu hulowekwa kwenye maji yenye nyuzi joto 14 CELSIUS.

Hatua hii hupelekea kuzalishwa kwa kimea ambacho huhamishwa kwenye jokofu maalumu ili kikauke na mvuke upunguzwe kufikia 2%-4% ili kuzuia ukuaji zaidi.

Baada ya hapo kimea huchambuliwa ili kutoa mimea yoyote iliyokua kipindi cha kuloweka na baadaye kusagwa na kutunzwa tayari kwa ajili ya hatua ya pili.

2. KUTENGENEZA KINYWAJI

MUDA: Masaa 6-10

Hatua hii inalenga kutengeneza kinywaji kitamu kwa kutumia vimeng’enya (enzymes).

kimea kilichosagwa huchanganywa na maji na kupashwa joto hadi kufikia kiwango fulani maalumu kwa ajili ya kufanya vimeng’enya viweze kubadili wanga kutoka kwenye nafaka kuwa sukari rahisi (simple sugars)

Baada ya kama masaa manne kinywaji hiki huchujwa na kuondolewa makapi kisha huchemshwa ili kuzuia vimeng’enya visiendelee kubadili wanga kuwa sukari.

Wakati kinachemka maua ya mihopi huchanganywa ma kwa pamoja huchemshwa kwa masaa kama mawili hivi. Hatua hii ndiyo huipa bia ladha ya uchungu ambayo hutoka kwenye mihopi.

Baada ya hatua hii bia hupoozwa hadi kufikia nyuzi joto zinazohitajika tayari kwa hatua inayofuata.

Glasi ya bia kwenye kiwanda cha bia

3. UCHACHISHAJI

MUDA: Hadi wiki 1

Lengo la hatua hii ni kutengeneza KILEO (Alcohol).

Hamira huwekwa kwenye kinywaji kilichotengenezwa kwenye hatua ya pili ili kubadilisha sukari kuwa kileo na gesi ya Carbon dioxide.

Aina tofauti za bia zinatokana na utofauti katika muda wa kuchachisha pamoja na nyuzi joto za uchachishaji. Kwa hiyo viwanda mbalimbali vya bia huweza kutumia utofauti katika hatua hii ili kufanya bia zao ziwe na ladha na ubora wa aina ya kipekee.

Mwisho wa hatua hii bia huhifadhiwa kwenye matanki ili iendelee kukolea.

4 . UKOLEZAJI

MUDA: wiki 3- miezi kadhaa

Lengo la hatua hii ni kuipa bia ladha, harufu na mapovu kutokana na gesi ya Carbon dioxide.

Hatua hii tena inaweza kutengeneza utofauti kati ya aina mbali mbali za bia kupitia muda wa ukolezaji.

Baada ya bia kufikia kiwango sahihi kutokana na mtengenezaji huwekwa kwenye mapipa ya kusafirishwa au kuwekwa kwenye chupa tayari kwa kusambazwa.

Hivi ndivyo kwa kifupi tu jinsi bia zinavyotengenezwa.

Katika sehemu ya pili ya makala hii utaona ni jinsi gani unywaji wa bia husababisha kuongezeka uzito wa mwili au kuongezeka kwa kitambi.

SEHEMU YA PILI

You may also like...

2 Responses

  1. Love d agogo says:

    Thank you

COMMENT