MAZOEZI YA KUPUNGUZA UZITO NDANI YA WIKI 6 KWA KINA MAMA

Makala hii ni mwongozo kwa ajili ya wale wenye kitabu cha WIKI 8 FIT MAMA CHALLENGE.

BONYEZA PICHA KUPATA NAKALA YAKO!

Usisahau kujinyoosha na kupasha mwili joto (warm ups) kabla haujafanya mazoezi haya.

Ndani ya wiki sita mwili wako utakuwa umepiga hatua kubwa kuelekea kurudi kwenye saizi yake ya mwanzo!

Usikose kufanya mazoezi kwa kufuatilia mlolongo wa kwenye kitabu!

1. SQUATS

Mwanamke anafanya zoezi la squats

2. PUSH UPS

zoezi la push up kwa ajili ya kupunguza unene wa mikono na tumbo

Anza na hizi push up za magoti hadi utakapojisikia tayari kuendelea na push up kamili.

push up kwa ajili ya kupunguza mikono

3. KNEE- ELBOW SQUATS

Zoezi la knee elbow squat kwa ajili ya kuondoa tumbo

Zoezi hili ni zuri sana kwa ajili ya kupunguza tumbo kwa kukaza misuli . Ili kuepuka kuumia usichuchumae chini sana.

Anza taratibu na unapozoea jaribu kuchuchumaa chini zaidi.

4. PLANK

zoezi la plank kwa ajili ya kupunguza tumbo kwa wamama wanaonyonyesha
PLANK 1

Zoezi hili ni maarufu kwa ajili ya kupunguza mikono na tumbo.

Chagua moja kati ya haya mawili kisha ganda kwenye pozi hili kwa sekunde zilizoelekezwa kwenye kitabu.

Tumia stop watch ya kwenye simu yako kuhesabu sekunde au muombe mtu akuhesabie muda wakati wewe unaendelea.

mazoezi ya tumbo la uzazi
PLANK 2

5. BRIDGES

mazoezi ya kukaza tumbo baada ya kujifungua

Zoezi hili ni namba moja katika kusaidia kupunguza tumbo au kukaza misuli ya tumbo baada ya kujifungua.

Fanya taratibu ili upate matokeo mazuri zaidi. Tumia jamvi la mazoezi kwa ajili ya mazoezi yote ya kulala chini.

6. SPEED SKATERS

zoezi la kupunguza uzito
SPEED SKATER ORIGINAL

Original ni kwa ajili ya wanaojiona wana uwezo wa kufanya zoezi hili.

Zingatia kuruka umbali mkubwa pia pia kuinuka na kunyooka kabisa wakati wa kuruka au baada ya kugusa kidole.

Kama hauwezi kufanya zoezi hili kama inavyooneshwa hapo unaweza kulirahisisha kama ifuatavyo.

SPEED SKATER ILIYORAHISISHWA

Kama unavyoona hapa haugisi chini au vidole kwa hiyo ni rahisi zaidi kwasababu hauinami.

Fanya kwa kasi yako ili mradi ufikishe idadi ya siku kulingana na plan ya mazoezi ya kwenye kitabu.

Kufanya mazoezi haya kwa kufuatilia mpangilio wa kwenye kitabu pamoja na mpangilio wa chakula kutakufanya upunguze uzito vizuri na kudikia malengo yako haraka zaidi!

You may also like...

4 Responses

 1. Evelyne Mhina says:

  This is wonderful Hali…kitafatatilia huo mtiririko

 2. LAMU says:

  Hello Dada nimeanza kukufatilia na nimeona umuhim sana wakupata kitabu chako, nilikua naangalia haya mazoezo nikaona sit ups hukuweka hivo naomba kujua jee haisaidii kuondoa tumbo ? ama hayo ulioweka hapo ndio mazuri zaidi

  • GigiMaenda says:

   Hi dear! Karibu sana. Ni kweli watu wengi huamini sit ups ndiyo zoezi kuu la kupunguza tumbo lakini si sahihi 100%. Sit ups nzuri labda kwa ajili ya mtu ambaye tayari ni fit, hana mafuta mengi tumboni na anataka six packs. Lakini kwa wenye tumbo kubwa ni muhimu kuchanganya mazoezi mengine ya tumbo pamoja na mazoezi ya kuchoma calories (cardio excercises). Kwenye kitabu kuna maelekezo mazuri sana ya jinsi ya kufata mtiririko wa haya mazoezi na jinsi ya kula. Yaani matokeo yake yata ku-surprise!.

   https://gigimaenda.co.tz/jinsi-ya-kupunguza-tumbo-baada-ya-kujifungua/ unaweza fata hii link kuona mazoezi mengine muhimu ya tumbo ambayo hayajumuishi sit ups pia. Kitabu unapata Whatsapp 0714 975504 karibu sana dear!

COMMENT