MAKOSA MAKUBWA 5 YANAYOKUFANYA USIPUNGUE UZITO

Kuna baadhi ya watu wanafanya diet na mazoezi kila kukicha halafu aidha hawapungui au wanaongezeka na kupungua kilo zile zile miaka nenda rudi!

Mmoja kati ya watu hawa alikuwa ni mimi kusema kweli  Katika miaka yote minne nimeweza kupunguza 36 kg lakini ndani ya miaka mitatu nilikuwa ninapungua kilo 20 zile zile!.

Yaani nilikuwa ninapungua nakuongezeka tu, kama unachukua hatua tatu mbele halafu nne nyuma,  unaenda mbele tena na kurudi mwishowe unaishia pale pale!.

Baada ya kugundua makosa yaliyokuwa yananifanya nisipungue zaidi nilifanya mabadiliko na nikandelea kupunguza Kg 16 nyingine.

Hizi ndizo sababu zinazofanya watu wasifikie malengo yao ya kupunguza uzito kwa kudumu.

1. KUFATA DIET ZA SHORTCUT

Watu wengi wanapenda matokeo ya harakahivyo tunaishia kujikita kwenye diet fupi fupi kama cabbage soup diet, militarydiet, egg diet, yoghurt diet, boiled potato diet na nyingine nyingi sana.

Hizi diet zote zimeeleza kabisa kwamba siyo za kuzifatilia kwa ajili ya kupunguza uzito kwa kudumu. Na zote zinaeleza wazi kwamba usifanye zaidi ya muda fulani kama siku 4-10. Lakini kwa sababu wengi tunapenda matokeo ya ghafla tunang’a ng’ania badala ya kutumia muda mwingi zaidi kujifunza jinsi ya kula kwa afya kwa kudumu /healthy eating.

Hii inasababisha kupungua na kuongezeka tu tena wakati mwingine unaongezeka mara nne yake.

Diet fupi zitumike kama emergency mfano una tukio kama sherehe ndani ya siku chache na unataka kupungua kidogo nguo ikae vizuri, au kama detox tu ushtue mwili wakati wa kuanza healthy lifestyle yako.

Ukimaliza hizo siku za diet endelea na mlo uliokamilika ili uendelee kupungua kwa usahihi.

2. MATATIZO YA KIAFYA

Kama nilivyosema kwenye post kuhusu hatua 5 za kufata kabla haujaanza diet yoyote kupunguza uzito wa mwili, kuna baadhi yamatatizo yanaleta aidha urahisi wa kuongezeka uzito  au ugumu wa kupunguza uzito.

Kwa sisi wanawake mfano mzuri ni ugonjwa wa PCOS (Kama hauufahamu niachie ujumbe niandae makala ya undani zaidi juu ya ugonjwa huu), depression/msongo wa mawazo , matatizo ya tezi la Thyroid n.k.

3. KULA ZAIDI YA KIWANGO

Wengi baada ya muda fulani kwenye weightloss journey zao huwa wana relax! Mwanzoni unaanza vizuri kwa kupima chakula kwenye food scale, kuhesabu kalories au kuwa makini tu na kiasi unachopakua.

Baadaye aidha unachoka au unaona umekishazoea na unajua kukadiria kwa macho kwa hiyo unaachakupima inavyostahili. Hii inasababisha  kurudia tena ile tabia ya kula sana bila kujitambua.

4. KUTOFANYA MAZOEZI

Inafika wakati mwili wako unazoea mabadiliko yako ulaji wa kupunguza uzito kwa hiyo automatically unafikia hatua ya kupingana na juhudi zako za kupunguza mafuta (plateau).

Hii ni kwasababu mwili unapata hofu kwa kudhani kuwa labda upatikanaji wa chakula umepungua kwa hiyo ili kukuokoa unaongeza bidii kwa kung’ang’ania mafuta yaliyo hifadhi kwenye stoo zake.

Ukifikia stage hii unajikuta unafata diet inavyotakiwa lakini haupungui kwa muda mrefu. Hapa sasa ndipo wengi huwa wanakata tamaa na kuachana na diet yenyewe.

Ukifikia stage hii ni cha kufanya ni kuongeza bidii ya mazoezi kawasababu italazimisha mwili kuyeyusha mafuta kutengeneza nguvu kwa ajili ya kukukimu wakati wa mazoezi.

5. KUJILINGANISHA NA WENGINE

Pale mtu anapoangalia wenzake wanapungua sana na yeye hapunguzi mara nyingi anajikia kukata tamaa na tunaanza kujipa visingizio kama “mimi kwanza kwetu wote wanene” “hapa nilipofikia inatosha”n.k.

Kila mwili wa mtu ni tofauti. Safari yako ni ya kwako, usikate tamaa kama mwili wako haupungui haraka au hauoneshi kirahisi pindi unapopungua.

Tumia safari za wengine kujifunza na kujipa moyo tu.

Usikate tamaa! Kama mimi ninaweza kwanini wewe ushindwe?

Hugs, GG!

You may also like...

1 Response

  1. Furaha says:

    Dawa iyo inapatikana wapi

COMMENT