KWANINI BAADHI YA WATU HULA SANA BILA KUONGEZEKA UZITO?

Kila mtu anamfahamu Yule mtu mmoja ambaye huwa hanenepi miaka nenda miaka rudi!, anaonekana anakula kwa kiasi kikubwa cha chakula tena mara nyingi anaonekana anakula zaidi yako wewe ila wewe unaongezeka uzito wakati mwenzako haongezeki hata kilo moja! Tena kwa usalama wako unaona bora usimfatishe kiasi chake cha ulaji maana ukijaribu kumkaribia hata kidogo tu ni balaa!

Hapa nimeandaa hiki kipengele maalumu kwa ajili ya kujibu swali hili ambalo linasumbua akili za watu wengi!

Hizi ni baadhi ya sababu zinazosababisha baadhi ya watu kula sana bila kuongezeka uzito!

  1. WANAKULA CHAKULA KINACHOKIDHI MAHITAJI YA MIILI YAO:

eating

Kuna kiwango cha chakula kinachohitajika kwa binadamu kwa siku kutokana na Jinsia na umri (RECCOMENDED DAILY ALLOWANCE).

Ukizidisha kiwango hiki miili yetu hubadilisha kile kilichozidi na kukihifadhi kama mafuta hivyo kufanya mtu kuongezeka uzito/kunenepa.

Kwahiyo unaweza kuona mtu anakula sana lakini kutokana na umri, jinsia yake na shughuli anazofanya kile chakula hakizidi kiwango chake cha chakula kwa siku ndiyo maana haongezeki uzito.

2.WANATUMIA NGUVU NYINGI ZAIDI:

active

Watu hawa mara nyingi wapo active bila kudhamiria , wanatembea badala ya kutegemea sana vyombo vya usafiri, wanafanya kazi wenyewe badala ya kutuma tuma watu wengine, mara nyingi huwa wamesimama badala ya kukaa, au hujishughulisha mara kwa mara.

Kutokana na hili chakula chote wanachokula hutumika ipasavyo kuendeshea hizi shughuli ambazo ni za kawaida kwao, wala siyo mazoezi ya makusudi.

3. WANA ASILIMIA KUBWA YA MISULI MWILINI:

Uzito wa mwili wa binadamu ni mjumuisho wa uzito wa MAFUTA, MISULI, MIFUPA na MAJI.

Watu wenye asilimia kubwa na misuli huwa hata wakila chakula kingi mara nyingi nguvu zao huelekea kwenye kuikuza misuli hiyo na siyo kutengeneza mafuta.

Pia watu wenye misuli mingi zaidi kwa kawaida hutumia nguvu zaidi hivyo mara nyingi hata wakionekana wanakula sana chakula kile hutumika bila kubaki katika shughuli wanazofanya.

4. WANAFANYA MAZOEZI YA VIUNGO

Kuna watu huamua kula wanavyotaka ila wanahakikisha wanafanya mazoezi mara kwa mara ili kuhakikisha chakula wanachokula kinatumika badala ya kugeuzwa mafuta.

5. HAWALI SANA KAMA WEWE UNAVYODHANI

Ni ngumu sana kujua kwa uhakika kiasi gani mtu anakula asubuhi mchana hadi usiku! Labda kama unamfuatilia kwa masaa 24.

Watu wengi hudhani kuwa kuna watu wa aina yake ambao wao ni wembamba tu na hawanenepi hata wale nini.

Lakini ukifuatilia vizuri kiasi na aina ya chakula wanachokula, shughuli wanazofanya na kiasi cha misuli waliyonayo mara nyingi utagundua ukweli ni kwamba hawana sababu ya kuongezeka uzito kwasababu kiasi wanachokula kinawiana na mahitaji yao kuendana na umri, jinsia na shughuli wanazofanya.

You may also like...

COMMENT