KUNYWA MAJI YA MOTO NA LIMAO ASUBUHI HUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO?

Imekuwa ni kitu kinachofahamika sana kwenye ulimwengu wa diet na kupunguza uzito wa mwili kwamba mojawapo ya sheria muhimu ni kuhakikisha unakunywa maji ya limao kila asubuhi kabla ya kula kitu chochote.

Watu wengi wamekuwa wakifata sheria hii wakiamini kuwa kunywa maji ya uvuguvugu yenye limao husaidia kuyeyusha mafuta mwilini na hivyo kusaidia kupunguza uzito ipasavyo.

UKWELI:

Hakuna uhusiano kati ya maji ya vuguvugu yenye limao na uyeyushaji wa mafuta mwilini.

Imani hii iliibuka kutokana na tafiti iliyofanyika Japan (isome hapa) ambayo ililenga kugundua matokeo ya limao kwenye panya wenye uzito mkubwa au kiribatumbo.

Kulikuwa na makundi mawili ya panya waliolishwa vyakula vyenye mafuta mengi kwa makusudi ili waongezeke uzito au wanenepe. Kundi moja walipewa maganda malimao na kundi moja hawakupewa.

Baada ya muda wale panya ambao hawakulishwa malimao walionekana kuwa na uzito mkubwa zaidi kuliko wale waliokula malimao.

Hii ikasababisha watu kuamini na kusambaza taarifa kwamba kunywa maji yenye limao kunapunguza uzito wa mwili na kuzuiz unene uliopitiliza (kiribatumbo).

HITILAFU:

  • Tafiti ilifanyika kwenye panya na si binadamu.
  • Panya hawa walikuwa wanakula maganda ya limao yaliyosagwa na siyo juisi ya limao . Kukamua limao tu na kuchanganya na maji tayari kunapunguza virutubisho vingi ambavyo vinapatikana kwenye malimao.
  • Kiasi cha maganda ya limao walichokuwa wanakula panya hao ni kikubwa sana ambacho binadamu akijaribu kukifatisha atapata madhara makubwa kutokana na ACID iliyopo kwenye malimao.

Maji ya uvuguvugu yenye limao yanawezaje kusaidia kupunguza uzito wa mwili?

  • Yanaongeza ladha ya maji hivyo kukusaidia kunywa maji mengi na kuongeza maji mwilini.
  • Utajisikia umeshiba ukinywa maji mengi hivyo hautakuwa unakula sana.
  • Ukinywa maji mengi hamu ya kula inapungua.

Ukitaka kupunguza uzito wa mwili zingatia kubadilisha mfumo wako wa ulaji ili upate matokeo mazuri na ya muda mrefu.

Tumia maji ya uvuguvugu yenye limao kama nyenzo ya kukusaidia kupunguza kula sana na kunywa vinywaji vyenye sukari kama soda sio kama nyenzo ya kuyeyusha mafuta mwilini.

Soma makala zifuatazo kukusaidia kupunguza uzito wa mwili wako kiusahihi.

You may also like...

2 Responses

  1. Raniyah Anwar says:

    Hehe very interesting hata na mm nliamini inapunguza uzito.

COMMENT