JINSI YA KUPUNGUZA UZITO KWA KUNYWA MAJI

Watu wengi hudhani ni ngumu sana kupunguza uzito kwasababu huwa wanapata wakati mgumu kubadilisha mfumo wao wa ulaji na kufata diet ya kupunguza uzito.

Ukweli ni kwamba kuna njia ambazo ni rahisi tu zinazoweza kukupa nafasi ya kuwa na mwanzo mzuri na mrahisi katika safari yako ya kupunguza uzito.

Njia mojawapo rahisi sana ya kupunguza unene ni kuongeza kiasi cha maji unayokunywa kwa siku.

Wanasayansi bado hawajatambua kiundani zaidi jinsi maji yanavyosababisha kupunguza uzito wa mwili lakini kuna tafiti nyingi sana ambazo zinaonesha kuwepo na uhusiano mkubwa kati ya kunywa maji mengi kupungua kwa uzito wa mwili.

SOMA JINSI MAJI YANAVYOSABABISHA KUPUNGUA UZITO HARAKA!

Mwanamke anakunywa maji

Mtindo wa unywaji maji ambao unatambulika kisayansi kusaidia kupunguza uzito haraka zaidi ni kunywa lita moja na nusu ya maji kabla ya kula milo yote ya siku.

Tafiti zinaonesha kwamba watu wazima wanaokunywa nusu lita ya maji ndani ya dakika 30 kabla ya kula kifungua kinywa, chakula cha mchana na chakula cha jioni hupunguza uzito kwa 40% zaidi ya watu wasiofata mtindo huu wa kunywa maji.( 1 )

Hii ina maanisha kama lengo lako ni kupunguza uzito wa kilo 20 basi kilo 8 kati ya hizo zinaweza kupungua kupitia wewe kunywa nusu lita ya maji kabla ya kula chakula bila kusahau kuendelea kunywa maji mengi ndani ya siku nzima.

Katika tafiti nyingine wanawake 50 waliokunywa nusu lita ya maji kabla ya kula walionekana kupunguza kiasi cha mafuta mwilini na kupunguza hamu ya kula kuliko wale ambao hawakufata mtindo huu ( 2 )

Kama unapata shida ya kupunguza uzito kwasababu una tatizo la kula chakula sana au kushindwa kujizuia kila unapoona kitu cha kutafuna…

SOMA: JINSI YA KUACHA KULA SANA NA KUANZA KUPUNGUZA UZITO LEO.

Kunywa maji ya kutosha pamoja na kunywa kabla ya kula hupelekea kupungua kiasi mafuta mwilini kwasababu maji huongeza uwezo wa mwili kutumia malighafi kwa kuchoma calories kwa ajili ya kutengeneza nguvu. ( 3 , 4 , 5 )

Kwa kifupi kunywa maji mengi wakati ukiwa unafata mpangilio wa chakula au diet ya kupunguza uzito hupelekea kupunguza uzito mkubwa kwa muda mfupi zaidi kuliko kufata diet bila kunywa maji.

Na ndiyo maana diet nyingi zinasisitiza mazoezi kwasababu mazoezi huleta kiu hivyo kufanya unywe maji zaidi.

Kama unatamani sana kupunguza uzito wa mwili wako basi anza leo kunywa maji mengi pamoja na kunywa nusu lita ya maji kabla ya chakula na utashangaa matokeo mazuri utakayoyaona ndani ya muda mfupi tu!

JINSI YA KUFAHAMU KAMA UNA UZITO ULIOPITILIZA

PUNGUZA HADI KILO 5 NDANI YA WIKI: DIET YA SUPU YA KABICHI

MAZOEZI 5 YA KUPUNGUZA TUMBO HARAKA BILA GYM WALA VIFAA

You may also like...

COMMENT