JINSI YA KUPUNGUZA UZITO HARAKA KWA KULA VYAKULA VIBICHI.

Diet ya vyakula vibichi haikuwa inafahamika sana hapo zamani lakini katika miaka ya hivi karibuni imepata umaarufu mkubwa sana duniani kutokana na watu wengi kutoa shuhuda za kupunguza uzito mkubwa sana kwa kuifata.

Diet hii inasaidiaje kupunguza uzito wa mwili?

 1. CALORIES CHACHE: Tunapopika chakula huwa tunaongeza vitu kama mafuta, tui la nazi, karanga na vitu vingine vingi ambavyo hufanya chakula kiwe na calories nyingi zaidi hivyo kuweza kusababisha kupitiliza kiasi cha calories tunazohitaji kwa siku.
 2. KIASI KIKUBWA CHA NYUZI NYUZI (FIBRE): Vyakula vibichi vina nyuzi nyuzi nyingi zaidi na ambazo hazijalainishwa na moto. Hii hufanya mwili wako kuhitaji muda mwingi zaidi kuzimeng’enya tumboni hivyo kupelekea kujisika umeshiba kwa muda mrefu zaidi.
 3. RAHISI KUIFATA: Watu wengi wanapopewa meal plans kwa ajili ya kupunguza uzito mara nyingi hulalamika kuwa wanashindwa kufata recipes na kupika vyakula wanavyotakiwa kula. Diet hii haileti hilo tatizo, hata wasiojua kupika wanaweza kuifata kwasababu inahitaji maandalizi madogo tu
 4. INAOKOA MUDA: Kwasababu chakula hakipikwi, muda unaotumika ni kuandaa tu.
 5. VIRUTUBISHO VINGI ZAIDI: Kupika chakula mara nyingi huharibu baadhi ya virutubisho. Kula vyakula vibichi humaanisha unapata kila kirutubisho katika hali yake ya halisi.

KUMBUKA: Kupika chakula ni muhimu pia kwa ajili ya kuactivate baadhi ya enzymes kwa ajili ya mmeng’enyo wa chakula.

Kwasababu siyo rahisi kuanza kuifata diet hii 100% ni vizuri kuanza na 50/50 halafu unaweza kuongeza kiasi kutokana na matokeo ya kupungua uzito yanavyoendelea.

JINSI YA KUANZA KUPUNGUZA UZITO KWA KUTUMIA VYAKULA VIBICHI

Vyakula unavyoweza kula ni kama vifuatavyo

 • Mboga mboga (Vegetables) : Nyanya, Carrot, pili pili hoho, matango, zuccini, baby spinach nk.
 • Matunda: Apples, strawberries, zabibu, ndizi, maembe, mapapai,matango nk
 • Karanga: Almonds, walnuts,korosho, macadamia, pecans nk
 • Mbegu: Chia seeds, mbegu za maboga, mbegu za alizeti nk
 • Nafaka: Oats
 • Maziwa: Maziwa ya Almond, ya soya, ya oats nk (ya ng’ombe yachemshwe)

JINSI YA KULA

Kwasababu unaanza 50/50 hakikisha nusu ya vyakula unavyokula katika siku ni vibichi.

ASUBUHI:

SMOOTHIE: Blend maziwa, tunda mf ndizi, baby spinach na kijiko cha chia seeds.

AU

SALAD YA MATUNDA: Apple, tikiti maji, nanasi, matango, parachichi nk

AU

OATS ZA KULOWEKA: Usiku chukua oats changanya na maziwa na tunda unalopenda kisha weka kwenye fridge ule asubuhi kama breakfast.

MCHANA

VEGGIE SALAD: Changanya Matango, nyanya, kitunguu, pilipili hoho, karanga kidogo na vijiko vichache vya maharage meusi yaliyochemshwa.

USIKU

Wali wa brown kidogo na samaki wa mchuzi pamoja na mboga za majani kwa wingi.

AU

Ugali kidogo, chicken breast/kuku (bila ngozi) na mboga za majani kwa wingi

Jaribu kufuata mifano hii ukiongeza na mingine utakayoipata na utaona matokeo makubwa katika kupungua uzito wa mwili wako.

Jumuisha na mazoezi ya viungo ili kuharakisha matokeo yako na kukufanya ujisikie vizuri zaidi.

Kumbuka kuosha vizuri mbogamboga zako na matunda kwa kutumia maji safi yanayotiririka siyo kwenye bakuli.

Osha kwa kutumia maji ya bomba au omba msaada wa kumiminiwa maji kwenye mboga wakati wewe unazisafisha.

Hii itasaidia kutoa uchafu wote na kuzifanya ziwe salama kwa kula.

Style hii ya kupunguza uzito haishauriwi kwa watu wenye matatizo ya afya makubwa/ya kudumu, wanawake wajawazito, watoto na watu wenye matatizo ya figo.

Bonyeza link zifuatazo ili kujifunza zaidi njia nyingine zitakazokusaidia kupunguza uzito wa mwili wako

You may also like...

COMMENT