JINSI YA KUPUNGUZA TUMBO BAADA YA KUJIFUNGUA

Ili kuondoa ukubwa wa tumbo baada ya kujifungua kwanza kabisa ni muhimu kuanza kula chakula ipasavyo ili kuweze kupata virutubisho vya kutosha kwa ajili ya mwili wako.Ukizingatia aina ya vyakula unavyohitaji kula pamoja na kiasi chake kwa siku basi hautakuwa na changamoto yoyote katika kupunguza tumbo lako!

SOMA: JINSI YA KUPUNGUZA TUMBO KWA WAMAMA WANAONYONYESHA

MAZOEZI YA KWA AJILI YA KUPUNGUZA TUMBO

1. KUTEMBEA

Moja wapo ya njia nzuri na salama zaidi ya kuanza kupunguza tumbo baada ya kujifungua ni kutembea.

Tofauti ma mazoezi mengine, unaweza kuanza kutembea mapema zaidi baada ya kujifungua kwasababu haitasababisha mwili wako kupata madhara yananayoweza kutokana na kuchoka kwa kufanya kazi nzito.

Anza kwa kutembea taratibu kwa nusu saa kila siku. Unaweza kutembea kuzunguka nyumba yako au hata maeneo ya karibu na nyumbani.

Usijilazimishe kutumia nguvu nyingi sana, sikiliza mwili wako, unapoona unajisikia vibaya punguza mwendo upumzike.

Kutembea kutasaidia pia kuongeza mwendo wa kupona mwili wako hasa kwa wale waliojifungua kwa upasuaji au ambao walishonwa baada ya kujifungua kwa njia ya kawaida.

Kila unapozidi kupona na kujisikia nguvu zinaongezeka anza kuongeza mwendo na kuongeza muda au umbali wa kutembea hadi ufike sehemu unayoweza kuanza mbio za taratibu au jogging.

Kutembea husababisha mwili wako kutumia mafuta yaliyopo kutengeneza nguvu kwa hiyo ni aina ya mazoezi ambayo husaidia sana kupunguza uzito haraka.

MAZOEZI YA KUIMARISHA MISULI YA TUMBO

Wakati wa ujauzito tumbo linavyotanuka na misuli ya tumbo huvutika hivyo kuifanya ilegee kadri mtoto anavyozidi kuongezeka ukubwa.

Hivyo baada ya kujifungua ni muhimu sana kufanya mazoezi ya tumbo ili liweze kurudi katika hali yake ya mwanzo kabla ya mimba.

Kabla ya kuanza mazoezi haya ni muhimu kupasha mwili moto kwa kufanya mazoezi ya kujinyoosha ili kuepuka kuiathiri misuli zaidi.

2. PELVIC TILTS

Hili ni zoezi la kwanza kabisa kuanza nalo kwa ajili ya kupunguza tumbo au kukaza misuli ya tumbo baada ya kujifungua.

  1. Lalia mgongo kisha ukunje miguu magoti yawe juu na nyayo iwe sakafuni.
  2. Kwa kutumia misuli ya tumbo jinyanyue kiuno kidogo na ukivute kama unakielekeza ndani au kuelekea kichwani kisha ukirudishe tena chini.
  3. Rudia mara 10-15 hadi utakapoona unaweza kuongeza zaidi.

3. CRUNCHES

Hii ni aina ya zoezi muhimu sana kuanza nalo kwa ajili ya kupunguza tumbo baada ya kujifungua.

  1. Lala mgongo ukiwa kwenye sakafu kisha ukunje miguu kwenye magoti.
  2. Weka viganja vya mikono nyuma ya shingo kisha kaza tumbo na unyanyue kichwa na kifua kuelekea kwenye magoti kama unataka kuamka na kukaa.
  3. Usitumie mikono kujinyanyua bali tumia misuli ya tumbo.
  4. Anza kwa kufanya 10-15 kwa siku kisha ongeza pale utakapoona kiasi hiki kinakuwa kirahisi sana.

Wakati mwingine unapofanya cruches badala ya kuinuka moja kwa moja kuelekea kwenye magoti jikunje upande mmoja kama unataka kiwiko cha kulia kielekee kwenye goti la kushoto halafu cha kushoto kielekee kwenye goti la kulia.

Haya ndiyo mazoezi muhimu kabisa ya kuanza kupunguza tumbo baada ya kujifungua.

Kumbuka usiwe na haraka sana, anza taratibu na baada ya mwili wako kuwa vizuri kuanzia wiki 6-8 baada ya kujifungua ndiyo unaweza kuanza mazoezi.

SOMA ZAIDI

  1. NJIA 3 ZA KUPUNGUZA TUMBO HARAKA
  2. MAZOEZI 5 YA KUPUNGUZA UNENE WA MIKONO HARAKA
  3. JINSI YA KUPUNGUZA UZITO BILA DIET WALA MAZOEZI

ONA JINSI YA KUPIKA VYAKULA VYA WIKI NZIMA KWA AJILI YA KUPUNGUZA UZITO/TUMBO HARAKA

JINSI YA KUPIKA VYAKULA VYA DIET YA WIKI 1 KWA AJILI YA KUPUNGUZA UZITO / TUMBO HARAKA | Meal prep

You may also like...

COMMENT