JINSI YA KUJUA KAMA UNA UZITO ULIOPITILIZA AU OBESITY

Kisayansi tunatumia kipimo kinachoitwa BMI (Body Mass Index) ili kufahamu kama uzito wako unaendana na mahitaji ya mwili wako au la.

Katika kipimo hiki tunapima uzito katika Kilogram na urefu katika Mita (Metres) katika kanuni ifuatayo :

BMI= UZITO (kg)/ (urefu)(urefu)

Ina maana kama uzito wako ni Kg 100 na urefu wako ni Mita 1.65

100/((1.65)(1.65)) BMI yako inakuwa 36.7

Jibu utakalopata litakujulisha kama uzito wako ni mkubwa sana kwa kutumia sheria maalumu kama ifuatavyo.

  • 18.5 Kushuka chini = UZITO WA CHINI (UNDERWEIGHT)
  • 18.5 – 24.9 = UZITO WA KAWAIDA
  • 25 -29.9 = UZITO WAKUZIDI (OVERWEIGHT)
  • 30 – 34.9 = KIRIBATUMBO CLASS 1 (OBESITY CLASS 1)
  • 35 – 39.9 = KIRIBATUMBO CLASS 2 (OBESITY CLASS 2)
  • 40 Kwenda mbele = KIRIBATUMBO KILICHOPITILIZA (EXTREME OBESITY)

Kwa hiyo kama una Uzito wa Kilogram 100 na urefu wa Mita 1.65 BMI yako ya 36.7 inamaanisha wewe upo kwenye stage ya Kiribatumbo class 2.

Kuwa na uzito uliozidi kunapelekea matatizo mengi ya afya kama ilivyoandikwa kwenye makala ya jinsi unene unapelekea ugonjwa wa pressure ya kupanda na shinikizo la damu.

Kama BMI yako inaonesha kuwa uzito wako ni mkubwa sana, ni muhimu kuanza sasa hivi kufanya jitihada za kupunguza mafuta mwilini. Jifunze jinsi ya kuanza weightloss journey yako hapa na uanze kuishi maisha ya afya zaidi.

Kwa kutumia formula hii hii ya BMI pamoja na values zake unaweza kukokotoa uzito ambao ni wa sahihi kwako kutokana na urefu wako kama ifuatavyo.

Tukiendelea na mfano wetu wa mtu mwenye urefu wa Mita 1.65 kwa kuzingatia kuwa BMI sahihi ni kuanzia 18.5 hadi 24.9. Tunaweza kugeuza formula ili tupate uzito sahihi unaohitajika kwa mtu aliye na urefu huo.

UZITO = BMI ((UREFU)(UREFU))

UZITO =18.5((1.65)(1.65)) = 50.36

UZITO =24.9((1.65)(1.65)) = 67.8

Kwa hiyo mtu mzima mwenye urefu wa Mita 1.65 uzito wake wa kiafya anaotakiwa kuwa nao ni kuanzia 50kg hadi 67 kg

Jenga tabia ya kupima uzito ili kuwa makini usipate madhara ya unene uliopitiliza.

You may also like...

2 Responses

  1. festo says:

    Nzuri sana

COMMENT