JINSI YA KUEPUKANA NA KITAMBI CHA BIA: SEHEMU YA 3

Katika sehemu ya kwanza na ya pili tumeona jinsi bia zinavyotengenezwa na jinsi zinavyosemekana kusababisha kuongezeka ukubwa wa tumbo au kuongezeka uzito kwa kiujumla.

Soma sehemu ya kwanza hapa

Soma sehemu ya pili hapa

Kwahiyo sasa tunaenda kwenye sehemu muhimu kuliko yote nayo ni jinsi gani unaweza kuendelea kufuraia aina hii ya kinywaji bila kuwa na hofu ya kuongezeka uzito hasa kitambi.

1. PUNGUZA KIASI

Kama tulivyoongelea kwenye sehemu ya pili ya makala hii, chupa za ujazo mbalimbali za bia zina kiasi fulani za calories.

Kwa kuzingatia kuwa mwanamke anahitaji calories 2,200 na mwanaume 2,500 kwa siku ili ku-maintain uzito alionao utagundua kuwa ukipunguza kiasi cha bia unachokunywa kunasaidia kukuepusha kuongezeka uzito haraka.

2. LIGHT/LITE BEER

Hizi ni zile bia zilizopunguzwa kiasi cha kileo na wanga kwa ajili ya watu ambao wanataka kupunguza kiasi cha pombe wanachotumia au wale ambao wanataka kupunguza uzito.

JINSI LIGHT BEER ZINAVYOTENGENEZWA

Rejea hatua za kutengeneza bia kwenye sehemu ya kwanza ya makala hii. Katika hatua ya pili tumeona kuwa kimea hupashwa joto ili vimeng’enya maalumu vibadilishe wanga wa kwenye kimea kuwa sukari rahisi.

Katika kutengeneza light beer vimeng’enya/ enzymes huongezwa zaidi ili kuhakikisha wanga mwingi zaidi unabadilishwa kuwa sukari rahisi.

Baada ya hapa amira huongezwa ili kubadilisha ile sukari kuwa alcohol.

Matokeo yake ni kwamba kinywaji kinakuwa na wanga kidogo na kileo kingi kwasababu sukari ilikuwepo nyingi.

Ilikushusha kiasi cha kileo hatua inayofata ni kuongeza maji hadi ili kupunguza kileo.

Hapo ndipo inapotokea bia ambayo ina kiasi kidogo wanga na kileo kulinganisha na bia za kawaida.

Soko la light/lite beer limekua sana duniani kwasababu watu wengi wameathirika sana na tatizo la kuongezeka uzito hasa kitambi kutokana na kunywa bia.

Moja ya Lite beer nzuri na yenye ubora wa hali ya juu sana ni Serengeti Lite kutoka Serengeti Breweries Limited. Ukitumia hautajisikia kama unakunywa lite beer kutokana na ladha yake ilivyo karibu sana na ladha ya original Serengeti.

Bia hizi huwa na calories chini ya 100 na wanga kidogo hivyo kama unataka kupunguza uzito ni vizuri kutumia hizi kuliko bia za kawaida.

3. PUNGUZA CHAKULA WAKATI WA KUNYWA BIA

chupa za Bia na sahani ya nyama choma

Mara nyingi huwa tunapenda kula bia na vyakula hasa vyenye mafuta mengi kwasababu bia zinasemekana kuongeza hamu ya kula.

Pia kwasababu watu huwa ni ngumu kwa watu wengi kukaa tu bila kutafuna.

Mara nyingi ukiwa unakunywa haufikirii ni kiasi gani cha bia au chakula unaingiza mwilini mwako kwasababu alcohol hufanya mtu apoteze uwezo wa kujizuia kufanya vitu vingi.

MFANO:

Umeenda pub ukanywa bia 5 halafu ukaagiza na nyama choma ya ng’ombe nusu kilo pamoja na ndizi mbili za kuchoma.

Bia 1 chupa ya kawaida ya ml 350 ina calories 150- tuchukue wastani calories 160.

160 x 5 = 800

Nyama ya ng’ombe nusu ya kuchoma steki isiyo na mafuta = 1250

Ndizi mbichi 1 = calories 218 x 2 = 436

Bia 5 + nyama choma 1/2 kg + ndizi choma mbichi 2

800 + 1250 + 436 = calories 2268

Ina maana kama ni mwanamke tayari amekula zaidi ya kiasi cha chakula anachohitaji kwa siku ndani ya mlo mmoja tu!. Na kama ni mwanaume kabakisha calories 232 tu.

Kila calories zinazozidi zinahifadhiwa mwilini kama mafuta. Kwa hiyo kaa utafakari unakunywa bia ngapi na chakula kiasi gani.

Ukipunguza chakula au ukibadilisha aina ya chakula hapo unaweza kujiepusha na kuongezeka uzito.

4. FATA DIET SAHIHI

Chakula cha kupunguza uzito

Kama unajijua unapenda kunywa bia basi zingatia kula kwa kufata misingi ya afya na kula kwa malengo ya kukufanya usiongezeke uzito.

Hakikisha unakula mlo uliokamilika kabla ya kwenda kunywa sehemu. Hii itakufanya uwe umeshiba chakula chenye afya na chenye calories chache hivyo itakuzuia kula sana pale alcohol itakapo kuwa kwenye damu yako.

5. FANYA MAZOEZI YA VIUNGO

vifaa na viatu vya mazoezi

Mazoezi husaidia kutumia zile calories zilizopitiliza kutengeneza nguvu badala ya kwenda kukaa mwilini mwako kama mafuta.

Hakikisha unaratiba maalimu ya kufanya mazoezi, na hakikisha baada ya kunywa bia na kula sana kesho yake unafanya mazoezi mara mbili yake.

Kwa ufupi:

Kitambi hakisababishwi na kunywa bia tu. Vile vitu vingine unavyokula huku ukinywa bia vinaweza kuwa ndiyo visababishi vikubwa zaidi.

Kosa kubwa ni kwamba pombe inatumika kama kitu kinachojumuisha watu pamoja na kinaongeza hamu ya kula tu hivyo kusababisha calories nyingi kuliwa au kunywewa kwa muda mfupi.

Sio kila mtu anayekunywa bia ana kitambi kwasababu unaweza kubalance milo yako na kufanya mazoezi ili usiongezeke uzito.

Tumia mahesabu uliyoona kwenye makala hizi zote kabla ya kuanza kunywa bia , pia jifunze kula kwa afya ili ujiepushe na tatizo hili au ili urudishe mwili wako kwenye umbo lake la kawaida.

Kumbuka kuwa inawezekana! usije kujikatia tamaa na kudhani kuwa haiwezekani kwasababu tu wewe umejaribu mara nyingi umeshindwa.

Unaweza, kama unahitaji msaada usisite kuutafuta, afya yako ndio kitu cha muhimu kuliko vyote!.

You may also like...

COMMENT