JINSI UNENE UNAVYOSABABISHA SHINIKIZO LA DAMU NA MSHTUKO WA MOYO

Kiribatumbo (obesity) ni tatizo linalohusisha mtu kuwa na uzito uliozidi 20% ya uzito sahihi unaotakiwa kimisingi ya afya kutokana na urefu wake.

Kuwa na uzito mkubwa sana kuna madhara makubwa kwenye viungo vingi vya mwili sana sana moyo, ini, figo, mapafu, utumbo mpana, ngozi, mishipa ya damu na ubongo.

Madhara haya husababishwa kwanza kwa ile hali ya mafuta kuzunguka viungo hivi muhimu hivyo kuvikandamiza na kuvinyima nafasi.

Pili kitendo cha mafuta kuwepo ni hatari kwasababu katika hali ya kawaida ni kitu kigeni na hakitakiwi kuwepo mahali kinapojikusanya. Hii kusababisha mfarakano katika shughuli za kawaida za mwilini.

Tafiti zinaonesha kuwa watu wenye mafuta mengi tumboni/kitambi (Central obesity) wapo katika hatari kubwa zaidi ya kupata matatizo haya ya moyo na mzunguko wa damu.

Mojawapo ya sababu ni kwamba mafuta hukandamiza organs zilizopo tumboni hasa figo ambazo ni muhimu sana katika kuhakikisha pressure ya damu mwilini ipo kawaida.

Kuwa na ukubwa wa tumbo wa cm 102 na kuendelea kwa wanaume na 89 cm kwa wanawake ni ishara ya kwamba upo kwenye hatari ya kupata matatizo yanayosababishwa na unene wa kupindukia mfano pressure ya kupanda (shinikizo la damu), mshtuko wa moyo, kiharusi, kisukari type 2, matatizo ya ini na figo n.k

Jinsi ya kujua kama una tatizo la pressure ya kupanda au shinikizo la damu.

Pressure ya damu ya kawaida ni 100-140 (namba ya juu =Systolic pressure) chini ya 60-90 (diastolic pressure) mmHg.

Kuwa diagnosed na shinikizo la damu ni lazima kupima pressure kwa usahihi zaidi ya mara moja katika siku tofauti.

Average yake ikiwa 140-159 namba ya juu au ya chini ikiwa 90-99 hiyo ni hypertension STAGE 1.

Shinikizo la damu/Hypertension STAGE 2 inakuwa pale namba ya juu ikiwa kuanzia 160 na zaidi au ya chini ikiwa 100 na zaidi.

Normal 100-120/60-90 mmHg

Pre hypertension : 120-139/80-89 mmHg

Stage 1 hypertension: 140-159/90-99 mmHg

Stage 2 hypertension: 160>/100> mmHg

Unaweza kukubaliana na mimi kwamba asilimia kubwa ya watu unaowafahamu wenye tatizo hili la shinikizo la damu wana uzito mkubwa au ni wanene.

Hii si kusema watu wembamba huwa hawapati tatizo hili bali ni ishara kwamba kuna uhusiano mkubwa kati ya tatizo la unene na kupanda kwa pressure.

Kuna sababu zaidi ya moja zinazosababisha tatizo la kuongezeka kwa pressure ya damu au shinikizo la damu. Mojawapo ya vitu vinavyokuweka kwenye hatari ya kupata tatizo hili ni ni kuwa na mafuta mengi mwilini.

Kuwa na mafuta mengi mwilini kunavyopelekea mshtuko wa moyo.

Moja ya tatizo linalosababisha matatizo ya moyo na msukumo wa damu ni ni kuziba au kupungua kwa size ya mishipa mikubwa kwenye mwili inayoitwa “Arteries”. Hii ni mishipa inayotoa damu safi na yenye oxygen kutoka kwenye moyo kupeleka kwenye sehemu mbalimbali za miili yetu.

Tatizo hutokea pale mafuta na cholesterol vinapotuama kwenye kuta za mishipa hii kidogo kidogo hadi kusababisha kizuizi kikubwa kinachofanya damu ipate tabu kupenya na kuendelea na safari yake (Atherosclerosis).

Tatizo hili likitokea kwenye mishipa inayopeleka damu kwenye moyo husababisha kutokea kwa shinikizo la damu (heart attack) kwasababu moyo ni msuli na misuli yote huhitaji oxygen ili iweze kufanya kazi.

Dalili mojawapo ya mshtuko wa moyo ni maumivu kifuani (angina). Msuli wowote unapokosa oxygen ya kutosha hushindwa kufanya kazi vizuri hivyo kusababisha maumivu.

Kukosekana kwa oygen kabisa husababisha msuli huo kuacha kufanya kazi kabisa. Hivyo moyo huacha kusukuma damu na ndipo mtu anakuwa amepata shinikizo la damu.

Dalili nyingine za mshtuko wa moyo ni maumivu kwenye taya, shingo au bega, kupungukiwa pumzi, kuishiwa nguvu na kizunguzungu cha ghafla, kuchoka kusiko kwa kawaida,hisia ya kiungulia, kichefuchefu au kutapika, jasho linaloambatana na hisia ya baridi.

Suluhisho: Jinsi ya kujiepusha na tatizo shinikizo la damu na mshtuko wa moyo.

Kubadilisha mfumo wa maisha na kuishi kwa kuzingatia afya ya ulaji na mazoezi ya viungo ndiyo hatua inayofaa zaidi.

Unene uliopindukia husababishwa na kula chakula kingi kuzidi mahitaji ya mwili. Hivyo kupunguza kiasi cha calories unachokula kutasaidia kupunguza mafuta mwilini hivyo kukupunguzia madhara ya kiribatumbo.

Mafuta yanayotuama kwenye mishipa ya damu na kusababisha atherosclerosis sio cholesterol tu. Kuna aina nyingine yanayoitwa ‘triglycerides’ na haya husababishwa pia na kula vyakula vingi sana vya aina ya wanga.

Kiasi kikubwa cha pombe kinahusishwa sana katika kuongeza aina hii ya mafuta kwenye damu.

Kwa hiyo usifikiri kujiepusha kabisa na vyakula vya mafuta bila kucontrol vyakula vya wanga vitakuepusha kikamilifu kuzuia tatizo hili. Cha muhimu ni kula a balanced diet, vyakula vya wanga zisizokobolewa mf brown bread, dona, brown rice.

Ni muhimu kutotumia mafuta yanayotakana na wanyama na badala yake kutumia mafuta ya mimea kama ya alizeti, ya olive, n.k ambayo hayana cholesterol.

Jenga tabia ya kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kugundua tatizo mapema na kulichukulia hatua kabla halijafikia stage ya kuhatarisha maisha.

You may also like...

2 Responses

  1. Abisai says:

    Mweeeee, mambo ninmazuri, mpaka najihis nina shinikizo la damu, si kwa heat burn ile ya jana usiku, 3hr🙄

    • GigiMaenda says:

      Lol! Kweli tena watu wengi huwa wanahisi kama heart attack kwasababu ya heart burn tu!. Pole sana kwa kweli itabidi uwe na anti reflux meds sasa ili next time ikitokea usipate tabu. Ungekuwa home first aid majivu kidogo tu unakuwa okay kabisa!

COMMENT