NI KWELI BIA ZINASABABISHA KITAMBI?: SEHEMU YA 2

Baada ya kuona jinsi bia zinavyotengenezwa kupitia sehemu ya kwanza sasa utatambua kwanini bia hudhaniwa kusababisha kuongezeka kwa unene wa mwili hasa tumbo.

Bonyeza HAPA kama umekosa sehemu ya kwanza.

BIA ZINASABABISHAJE KUONGEZEKA UZITO?

1. CALORIES KWENYE BIA

Katika hatua ya mwisho wa utengenezaji bia virutubisho viwili vinakuwa ndani yake ambavyo ni WANGA (Carbohydrate kutoka kwenye shayiri) pamoja na KILEO au alcohol.

Vitu hivi viwili vina kiasi chake cha calories kutokana na kiasi kilichomo kwenye bia.

FAHAMU ZAIDI KUHUSU CALORIES HAPA

Hii inamaanisha bia zenye kiasi kikubwa zaidi cha kileo na wanga huwa na uwezekano mkubwa sana wa kusababisha mtu kuongezeka uzito pale zinapotumika kwa kiasi kikubwa.

Bia tofauti zina asilimia tofauti za alcohol lakini wa wastani bia moja ya size ya kawaida huwa na calories 140-180 .

Zenye size kubwa kama 500 ml ;

  • GUINESS 180 Calories
  • PILSNER 220 Calories
  • HEINEKEN 220 Calories

Kwa siku mwili wa mwanamke unahitaji si zaidi ya calorie 2,200 na mwanaume 2,500 ili kubaki katika uzito wake wa sasanau ku-maintain.

Kuzidisha juu ya kiwango hiki husababisha mwili wako kuchukua kile kilichoongezeka kukigeuza mafuta hivyo kukufanya uongezeke uzito na kuwa na muonekano wa kunenepa.

2. CALORIES KWENYE VYAKULA VINGINE

glasi ya bia na sahani ya chipsi na nyama ya kuku

Asilimia kubwa sana ya sehemu zinapouzwa bia zina huduma ya chakula pia. Kwasababu hii, imekuwa ni kawaida kwa mtu kuagiza chakula kama nyama ndizi au chipsi pale anapoenda kutembelea sehemu hizi kwa lengo la kunywa bia.

Zipo tafiti za kisayansi zinazoonesha kuwa kileo au alcohol huongeza hamu ya kula. Kwa hiyo ukichanganya na calories za kwenye bia na za kwenye vyakula vinavyoliwa wakati wa kunywa bia uwezekano wa kunenepa unazidi kuongezeka!.

glasi ya bia na sahani ya wali wa curry na kuku na sahani ya naan

3. KUONGEZEKA KWA UTENGENEZAJI WA MAFUTA MWILINI

Alcohol ni kama sumu kwenye damu kwa hiyo unapokunywa mwili wako hufanya juu chini kuitoa nje.

Kwasababu hii ini huanza kuwa busy kuivunja vunja kwa lengo la kuiondoa kutoka kwenye damu,

Kitendo hiki husababisha uzalishwaji wa nguvu kutoka kwenye hiyo alcohol inayovunjwa na ini.

Tatizo ni kwamba kwasababu bia zina wanga pia kwasababu unakunywa huku unakula vyakula vingine vyenye mafuta mengi na wanga pia. Hizo calories kutoka kwenye hivyo vyakula vingine zote hazitatumika kutengeneza nguvu.

Na kwa kawaida Calories zisizotumika kutengeneza nguvu hubadilishwa kuwa mafuta na hivyo kukufanya uongezeke uzito.

Pasipokuwa na alcohol mwili hutumia calories kutoka kwenye vyakula vyote kutengeneza nguvu badala ya kuzitunza kama mafuta.

KWANINI MAFUTA HUENDA KWENYE TUMBO?

Kuna vitu 3 muhimu vinavyosababisha mwili wako uweke mafuta kwenye sehemu fulani za mwili zaidi ya sehemu nyingine. Navyo ni

  • UMRI
  • JINSIA
  • HORMONES
  • URITHI

Kisayansi wanaume wenye umri mkubwa ndiyo huwa kawaida ya kutunza mafuta kwenye tumbo.

Kutokana na hormone za kike wanawake wana sehemu nyingi zaidi za kuhifadhi mafuta mfano kwenye mapaja, makalio na kifuani.

Wanaume wana misuli mingi kuliko wanawake hivyo sehemu rahisi zaidi ya mafuta kuwekwa ni tumboni.

Pia kuna vithibitisho kwamba kuwepo kwa watu wengi wenye vitambi kwenye familia au ukoo huongeza uwezekano wa mtu kupata kitambi hata katika umri mdogo.

JE UNAWEZA KUNYWA BIA NA USIPATE KITAMBI?

madhara ya unywaji wa bia katika uzito wa mwili

Ndiyo! katika sehemu ya tatu ya makala hii utaona namna ya kuendelea kunywa pombe bila kuhofia kuongezeka uzito na ukubwa wa tumbo!.

You may also like...

COMMENT