Home

Chakula: aina na kiasi!

Mwili wako unastahili mazuri yote unayoweza kuupatia!. Ili kupunguza uzito wako na kuwa na afya njema  kimwili na kiakili ni muhimu kula vyakula vyenye virutubisho sahihi na kwa kiasi sahihi! Jifunze kuhusu kanuni za Calories ili ujue ni aina gani ya chakula ule kwa wingi au aina gani upunguze kutokana na mahitaji ya mwili wako!.

Madhara ya uzito mkubwa

Mtazamo wa watu wengi ni kuwa kama kitu hakiumi basi hakuna tatizo. Utasikia watu wenye uzito uliopitiliza wakisema hawana tatizo lolote, pressure ipo sawa, hana kisukari, figo ipo sawa. Ukweli ni kwamba haya matatizo yatatokea tu!. Bora kujikinga mapema kuliko kusubiri hadi moyo,figo, ini na viungo vishindwe kustahimili.

Inawezekana, anza leo!

Watu wengi wanaanza na wanafanikiwa, usikubali kubaki na huzuni huku ukitamani kuwa na mwili size fulani. Cha muhimu ni kuacha kutamani na kuanza vitendo. Badili afya na muonekano wako kwa kufanya mazoezi yenye kulenga misuli maalumu kwenye sehemu mbalimbali za mwili wako…