JINSI YA KUPUNGUZA UZITO KWA KUNYWA GREEN TEA

Kama umewahi kujaribu kufanya jitihada za kupunguza uzito wa mwili wako basi tayari unafahamu kuwa karibu kila mtaalamu utakayeongea naye au kila diet plan/meal plan ambayo umeiona imekulazimu kutumia green tea.

Kama wewe ni mara yako ya kwanza kufanya tafiti kuhusu jinsi ya kupunguza uzito basi ninakuhakikishia kwamba utaendelea kukutana na green tea katika kila njia utakayoamua kutumia kupunguza uzito wako.

Watu wengi wanakunywa green tea kwa kusikia tetesi tu kuwa inasaidia kupunguza mafuta mwilini lakini hawana uhakika kama ni ukweli au la. Leo nitajibu swali hili ambalo linawakuta wengi.

TOFAUTI KATI YA GREEN TEA NA BLACK TEA

kikombe kimoja cha green tea kwa ajili ya kupunguza uzito

Kwa muonekano wa nje, majani haya aina moja ni ya kijani wakati aina nyingine ambayo ndiyo tuliyoizoea ni meusi.

Tofauti kuu ipo katika uaandaaji ambapo Majani ya chai meusi huwa yanaachwa yapitie hatua ya kuchacha au (fermentation) kama maziwa yanavyoachwa ya chache ili kutengeneza mtindi wakati majani ya kijani au green tea hayaachwi yachache.

Tofauti nyingine zipo katika ladha na baadhi ya virutubisho ambavyo tutaviongelea kwenye makala nyingine.

Baada ya kuchumwa shambani majani yanayotakiwa kutengeneza green tea hupelekwa moja kwa moja kukaangwa ili yasiharibike wakati majani yanayoenda kutengeneza majani ya chai meusi hufungashwa na kuhifadhiwa sehemu yenye hewa ili yachache hivyo kupelekea kubadilika rangi na kuwa meusi.

Kwanini green tea inafahamika zaidi kwenye kupunguza uzito wa mwili?

Majani ya chai ya kijani (green tea) yanafahamika sana katika ulimwengu wa kupunguza uzito kwasababu yakilinganishwa na majani meusi yana Kemikali fulani zinazoitwa Flavonoids na Caffeine ambazo zinajulikana kisayansi kama vitu vinavyosaidia kuufanya mwili uweze kutumia malighafi zilizonazo kama mafuta na sukari kwa usanifu zaidi ili kutengeneza nguvu.

Kwa hiyo hizi Flavonoids na Caffeine kwenye green tea husaidia sana katika kupunguza uzito wa mwili kwa kuupa mwili wako wepesi wa kuyeyusha mafuta mwilini ili kutengeneza nguvu ambayo unaweza kuitumia katika shughuli zako au katika kufanya mazoezi ya viungo.

Green tea pia ina kiasi kikubwa cha antioxidant inayoitwa EGCG (Epigallocatechin-3-Gallate) ambayo kupitia tafiti za kisayansi imeonesha kuwa ina manufaa makubwa sana katika;

 • Kuzuia kusambaa na kuziua seli za cancer (1, 2)
 • Kuzuia tatizo la uchovu uliopitiliza (3)
 • Kuua microbacteria na baadhi ya virusi )(4 5, )
 • Kulinda ini dhini ya magonjwa yanayosababishwa na mafuta mengi (fatty liver disease) ( 7, 8 )
 • Kuepusha baadhi ya makali kwenye ugonjwa wa Alhzeimer’s ( 9, 10 )

Je ni kiasi gani cha green tea kinahitajika kwa siku ili kukusaidia kupunguza uzito wa mwili wako?

kunywa maji ya moto kupunguza tumbo

Kunywa kiasi cha Millilita 350 (350 ml) za green tea kwa siku kumeonekana kupelekea kupungua uzito wa mwili. Tafiti moja ilionesha kuwa watu waliokuwa wanakunywa kiasi hiki cha green tea kila siku walipungua kg 1.3 katika kipindi cha wiki 12 bila kubadilisha aina wao wa ulaji (bila kubadilisha diet).

Jinsi ya kuandaa green tea kwa ajili ya kukusaidia kupunguza uzito.

 • Ili kupata kiasi kikubwa zaidi cha virutubisho vyote kwenye majani haya unatakiwa kuwa mwangalifu.
 • EPUKA kutengeneza chai na maji yaliyotoka kuchemka, badala yake, maji yakishachemka acha yapoe kwa dakika 10 ili yasiendelee kuunguza na kuharibu virutubisho vilivyomo kwenye majani.
 • Baada ya kupoa mimina maji kwenye chombo chenye tea bag yako ya green tea.
 • Iache kwa dakika moja au zaidi ili majani yachanganyike na maji hadi yabadilike kuwa ya kijani.
 • Tayari kwa kunywa.

Ili kukusaidia kupunguza uzito wa mwili wako kwa haraka zaidi epuka kutumia sukari nyingi kwenye green tea yako. Pia ambatanisha green tea na mazoezi ya viungo pamoja na kula mlo uliokamilika kulingana na mahitaji ya mwili wako.

Kwa ufupi:

Kunywa 350 ml za green tea kila siku kunapelekea kupunguza uzito kutokana na kuwepo kwa vichocheo aina ya Flavonoids na Caffeine ambavyo husaidia mwili wako kutumia malighafi zilizopo mfano mafuta kutengeneza nguvu.
faida za green tea katika kupunguza uzito au tumbo

You may also like...

2 Responses

 1. Benjamin says:

  Green tea naipataje

  • GigiMaenda says:

   Inapatikana kwenye maduka makubwa ila sana sana kwenye supermarket! Yaani ukiingia kwenye supermarket mbili hauwezi kukosa!

COMMENT