EPUKA VYAKULA HIVI KILA ASUBUHI KAMA UNATAKA KUPUNGUZA UZITO

Ni kweli siku njema huanza asubuhi. Hata katika harakati za kupunguza uzito hatua unazozichukua asubuhi ndiyo huamua siku yako itakuwa na mafanikio au la.

Mara nyingi watu wanaofanikiwa katika safari zao za kupunguza uzito ni wale wanaoanza siku zao kwa kufanya mazoezi asubuhi na kula kifungua kinywa sahihi.

Katika makala hii ninaenda kukutahadharisha kuhusu aina za vyakula ambavyo vimezoeleka sana katika jamii yetu na ambavyo vinachangia kwa kiasi kikubwa sana kurudisha nyuma jitihada za kupunguza uzito huku vikisababisha wengi kuongezeka uzito bila kujijua.

1. VITAFUNWA VYA NGANO

vifungua kinywa vinavyosababisha kuongezeka uzito

Kundi hili la vitafunwa ndiyo linaongoza kwa kupendwa kuliko kundi lingine lolote!

Mifano mikubwa ni

 • Chapati
 • Maandazi
 • Mikate
 • Half keki
 • Sambusa

Ubaya wa vitafunwa hivi ni kwamba ngano ni aina ya chakula cha wanga, na nina uhakika hadi sasa unafahamu kuwa vyakula vyenye asili ya wanga ndivyo vinafahamika sana katika kusababisha kuongezeka uzito.

Unapokula vyakula vya wanga unasababisha kongosho imwage homoni ya insulin kwenye damu.

Insulin inapokuwa kwenye damu huzuia mwili kuyeyusha mafuta na badala yake huufanya mwili utunze kile chakula kilichozidi kwa kukibadilisha kuwa mafuta hivyo kupelekea kuongezeka uzito.

2. VITAFUNWA VISIVYO VYA NGANO

Mfano vitumbua, katlesi za viazi, kachori n.k

Tatizo la vitafunwa kama vitumbua ni kwamba vina kiasi kikubwa sana cha wanga (hutengenezwa kwa mchele na sukari) na pia upishi wake ni wa kukaanga kwa mafuta mengi.

Pia kwa sababu ya size ndogo pamoja na utamu wa sukari mara nyingi utajikuta unakula kiasi kikubwa bila kujishtukia au kujisikia umeshiba sana.

Unapokula vitafunwa hivi mara nyingi utagundua kuwa huwa unashiba kwa muda mfupi tu na baadaye kidogo unaanzakujisikia njaa tena.

Hii ni kwasababu vyakula vya wanga vinameng’enywa kirahisi tumboni, kwa hiyo baada ya muda mchache tumbo linakuwa limehsamaliza kazi yake na kubaki tupu tena hivyo kukusababisha kuanza kuhisi hamu ya kula tena.

3. MIHOGO/VIAZI/MAGIMBI

Watu wengi huamini kula mihogo au viazi vya kuchemsha na chai husaidia kupunguza uzito kwa sababu ni vyakula vya asili.

Mihogo inakuzuia kupunguza uzito

Hii ni imani potofu kwasababu vyakula hivi ni vya wanga na kama ulivyoona hapo juu vyakula vya wanga vinasababisha kuongeza uzito kutokana na utengenezwaji wa Insulin mwilini.

4. KIPORO

Kiporo ni kifungua kinywa cha taifa!.

Watu wengi sana wana mazoea ya kula kiporo kiasi kwamba hupika chakula kingi cha usiku makusudi ili kibaki na kiliwe asubuhi pamoja na chai.

Ubaya wa hili ni kwamba kawaida yetu mara nyingi mlo wa jioni unakuwa na kiasi kingi cha wanga kama wali, makande, ndizi nk.

Hii inasababisha kuanza siku kwa kujaza kiasi kikubwa cha wanga tumboni hivyo kupingana na jitihada zako za kupunguza uzito.

Pia kula chakula kizito hivyo asubuhi mara nyingi hukufanya uanze kusikia usingizi ndani ya muda mchache tu!

Unaweza ukawa umegundua kwamba vyakula vingi vya wanga kama ugali hufanya upate usingizi mara tu baada ya kula!

Kwa hiyo kama unataka kuwa mwenye nguvu nyingi na mchangamfu asubuhi nzima basi ni muhimu kuepuka kuanza siku yako kwa ulaji wa aina hii.

5. CEREALS ZENYE SUKARI NYINGI

Hizi ni kama corflakes , coco pops, rice krispies ambazo huliwa pamoja na maziwa kama kifungua kinywa.

Tatizo la hizi ni kwamba

 • Zinatengenezwa kwa nafaka ambazo zipo kwenye kundi la vyakula vya wanga.
 • Aina nyingi huwa zinaongezwa sukari wakati wa kuzitengeneza viwandani.
 • Uandaaji wake unakulazimu uongeze sukari TENA kwenye maziwa ndipo ule hivyo kuongeza kiasi kingine cha wanga juu ya kiasi kikubwa ambacho tayari kipo.

Kama umesoma makala nyingine zozote katika blog hii utakuwa unajua kwamba tafiti nyingi sana za kisayansi zinaonesha kuwa vyakula vya wanga ndiyo namba moja katika kusababisha kuongezeka uzito na kupelekea matatizo mengi ya kiafya yanayosababisha na kuwa na uzito mkubwa wa mwili.

Kana kwamba haitoshi, vitafunwa hivi mara zote huliwa pamoja na chai ambayo hutengenezwa kwa kuongeza vijiko viwili na zaidi vya sukari (SUKARI = WANGA 100%) na wakati mwingine maziwa au vionjo vingine vyenye sukari zaidi kama unga wa chocolate mf MILO, CADBURY DRINKING CHOCOLATE nk.

vuakula vya kuepuka ili kupunguza uzito

Kama mwili wako unahitaji kiasi ‘X’ cha wanga kwa siku ili ku-maintain afya na uzito ulionao sasa, ukila vyakula hivi asubuhi unaweza kujikuta umeshapitiliza kipimo chako cha wanga cha siku nzima ndani ya mlo mmoja tu hivyo kukusababisha kuongezeka uzito kila kukicha huku ukibaki unashangaa kwanini unanenepa.

Ili kupunguza uzito ni muhimu kufanya mabadiliko makubwa katika chakula chako cha asubuhi hasa kwa kupunguza kiasi cha wanga.

Hii itakuhakikishia kuanza kupunguza uzito unaokusumbua na kurudisha afya ya mwili wako.

Makala inayofata itakuonesha ni vyakula gani uvitumie kwa kifungua kinywa ili uweze kuanza kupunguza uzito wako mara moja!

“Bonyeza hapa kusoma makala ya vyakula sahihi vya asubuhi vinavyosaidia katika kupunguza uzito haraka”

Asante sana kwa kusoma makala hii na kwenye comments tafadhali niambie ni kifungua kinywa kipi kati ya nilivyotaja ndiyo unakipenda sana na huwa unakula kiasi gani na mara ngapi kwa wiki!

You may also like...

2 Responses

 1. Sandra says:

  Hello Gigi, Ahsante sana kwa nakala hii.. Mimi ni kati ya watu ambao tunastruggle sana kupunguza kitafunio vya wanga asubuhi.. Nimekuwa kwa muda mrefu sana nikila Chapati na supu.. Ahsante kwa hii nakala na hata ile ya vya vyakula kwa kula asubuhi, rahisi kutengeneza.. Nimependa sana ile smoothie.. Ahsante kwa kuendelea kunipa moyo… though i still struggle but reading this is helpful.i am grateful.

  • GigiMaenda says:

   Hi Sandy! Haupo peke yako yaani kutokana na tamaduni zetu watu wengi wamezoea kunywa chai na vyakula vya wanga! Tuendelee kujipa muda kuzoea pamoja na kujifunza kutengeneza mbadala wa vyakula hivi ambavyo tumevizoea. Asante sana kwa kujifunza, ninafurahi sana kuwa umepata kitu.

COMMENT