DIET YA MAYAI YA KUPUNGUZA UZITO KWA SIKU 7

Diet ya mayai ni aina nyingine ya diet fupi inayofahamika sana katika kupunguza uzito.

Kama kawaida kwa diet zote fupi, hii pia imeundwa kwa ajili ya kusaidia kupunguza uzito mkubwa pale unapokuwa na dharura.

Hii ni diet fupi ya NNE kuandikwa katika blog hii. Kama bado haujazisoma basi ni vizuri kuzipitia zote ili kuangalia ipi inakufaa zaidi.

SOMA: DIET YA SUPU YA KABICHI

SOMA: DIET YA UKWAJU

SOMA: DIET YA MTINDI

Yaliyomo

 • Kiasi cha Kalori kwenye mayai
 • Faida za mayai
 • Jinsi ya kuanza
 • Vyakula vinavyoruhusiwa
 • Ratiba ya siku 7
 • Tahadhari

KIASI CHA KALORI KWENYE MAYAI

Mayai hupatikana katika ukubwa mbali mbali kwa hiyo kiasi cha kalori kinaweza kuwa tofauti kidogo.

Mayai madogo sana huanzia na kalori 53 wakati yale makubwa sana kama ya bata hufikia hadi calori 90 kwa kila moja.

Yai moja la ukubwa wa kati huwa na kiasi kifuatacho cha virutubisho:

VIRUTUBISHOKIASI
Kalori 78
Protini 6 g
Mafuta 5 g
Wanga 0.6 g
Sukari 0 g
Cholesterol 0.19 g

Ni muhimu pia kufahamu kuwa kalori nyingi katika mayai zinapatikana kwenye kiini.

Kwa kawaida kiini huwa na asilimia 70 hadi 75 za kalori zote kwenye mayai.

Kwa hiyo unapoondoa kiini kabla ya kula mayai unapunguza kiasi kikubwa sana cha jumla ya kalori unazokula.

FAIDA ZA MAYAI

diet ya siku 7

Watu wengi huogopa kula mayai kwasabu ya imani kwamba yana kiasi kingi cha cholesterol ambacho hupelekea matatizo ya moyo.

Imani hii imeshapingwa mara nyingi sana kwa kupitia tafiti nyingi za kisayansi zinazoonesha kuwa cholesterol ya kwenye mayai haina madhara kama yalivyokuwa yakifikiriwa.

Tena tafiti hizi zinaonesha kuwa mayai yana faida nyingi katika mwili wa binadamu kama ifuatavyo.

PROTINI

Aina hii ya kirutubisho ni muhimu sana kwa afya ya viumbe hai kwasababu ya kazi yake ya kujenga mwili na kukarabati hitilafu zinazojitokeza.

Protini pia hutumika kutengeneza vichochezi au hormone, antibodies kwa ajili ya kinga ya mwili pamoja na enzymes.

Hivi vyote ni muhimu sana katika kuhakikisha miili yetu inakua na kufanya kazi kwa usahihi.

Kiasi cha protini unachotakiwa kula kwa siku mara nyingi hutegemea na uzito na urefu wako.

Lakini kwa kuangalia uzito tu, unahitaji gramu 0.8 ya protini kwa kila kilo moja ya uzito wako.

Ina maana mtu mwenye kilo 70 anahitaji gramu 70 za protini kila siku. Wale warefu zaidi huhitaji ziadi ya hapo kulingana na kimo chao.

MAFUTA

Karibia nusu ya kalori zilizopo kwenye mayai zinatokana na mafuta ambayo yapo kwenye kiini.

Sio kila aina ya mafuta ni mabaya kwa afya.

Yai moja lina kiasi cha gramu 5 za mafuta. Katika hizi yapo mafuta ambayo ni muhimu kwa afya yanayojulikana kama omega-3.

Kiasi kidogo sana (7%) kilichobaki ndiyo cha mafuta ambayo yanaweza kuwa si mazuri sana kwa afya.

CHOLESTEROL

Watu wengi huamini kuwa cholesterol ni kitu kibaya tu.

Hii si kweli kwasababu kirutubisho hiki ni muhimu sana katika miili wa viumbe hai.

Pia cholesterol iliyopo kwenye vyakula si lazima ipandishe cholesterol ya kwenye damu ( 2 , 3 )

Zipo kazi nyingi sana zinazofanikishwa na kirutubisho lakini baadhi yake ni kama kama zifuatavyo

 • Kujenga kuta za seli zote za mwili
 • Kutengeneza homoni hasa zile za uzazi
 • Kusaidia ini kutengeneza nyongo
 • Kusaidia utengenezwaji wa Vitamin D

CHOLINE

Hiki ni kirutubisho muhimu sana ambacho watu wengi hawakifahamu.

Choline sio vitamin wala si madini lakini mara nyingi hujumuishwa pamoja na kundi la vitamin B complex.

Kirutubisho hiki kinahusika na kazi mbali mbali mwilini hasa katika kutengeneza kuta za seli, kuimarisha shughuli za mfumo wa mishipa ya fahamu. ( 4 )

Choline inapatikana katika vyakula mbali mbali lakini kiini chai kinaongoza kwa kuwa na kiasi kikubwa sana.

Sehemu hii ya yai ina kiasi cha mg 680 za choline katika kila m g 100.

VITAMIN NA MADINI

Mayai ni chanzo kizuri cha vitamin na madini mbalimbali kama ( 1 )

 • Vitamin A
 • Vitamin B2, B7, B9, B12
 • Vitamin D
 • Vitamin E
 • Selenium
 • Calcium
 • Iodine
 • Phosphorus

Kiasi kikubwa cha vitamin zilizo kwenye mayai (kasoro vitamin B2) hupatikana kwenye kiini.

JINSI YA KUFATA DIET YA MAYAI KWA AJILI YA KUPUNGUZA UZITO

Punguza unene haraka

Zipo aina nyingi za diet ya mayai lakini hii ndiyo nzuri zaidi kwasababu inajumuisha aina nyingine ya vyakula.

Ipo aina moja ambayo inalazimu mtu kula mayai tu ndani ya siku zote saba kitu ambacho si kizuri kwa afya.

Kwa hiyo kama umepanga kujaribu diet hii ni vizuri kama utafata maelekezo katika makala hii na si mengine yenye sheria kali zaidi.

Kama kawaida diet hii inatakiwa kufatwa kwa siku 7 tu na si zaidi ya hapo.

Hii ni kwasababu diet hii ni ya dharura kwa hiyo inalenga kukufanya ule kiasi kidogo cha chakula ili kupunguza uzito haraka kisha uendelee na lishe sahihi.

Ni vizuri kuanza kuifata kwa siku 3 kwanza na kuangalia mwili wako unavyojisikia.

Kama utaweza kuendelea basi malizia hadi siku 7 lakini kama utashindwa unaweza kuishia hapo.

VYAKULA VINAVYORUHUSIWA

diet ya mayai kwa kupunguza tumbo

Kama ulivyoona hapo awali, ipo aina ya diet ya mayai ambayo hairuhusu kula chakula chochote zaidi ya mayai.

Katika makala hii nimetafuta ile diet ya mayai inayoruhusu baadhi ya vyakula vingine ili kukuzuia kukinai na kukata tamaa kabla haujafikia malengo yako.

Vyakula unavyoweza kula ni kama vifuatavyo:

 • Mayai ya kuchemshwa
 • Viazi vitamu
 • Viazi mviringo
 • Salad
 • Matunda (Mf machungwa, matango,papai, tikiti maji, parachichi, berries, apple, mapeasi, mapeaches nk)
 • Nyanya
 • Nyama (za aina yoyote lakini chagua zisizo na mafuta)
 • Samaki
 • Mboga za majani
 • Green tea

RATIBA YA SIKU 7

SIKU YA 1

ASUBUHI

 • Mayai ya kuchemsha 2
 • Chungwa 1
 • Green tea kikombe 1

MCHANA

 • Viazi vitamu vya kuchemshwa vipande 2
 • machungwa 2

USIKU

 • Bakuli kubwa la salad / Kachumbari
 • Kuku 1/4 (au nyama ya aina nyingine)

SIKU YA 2

ASUBUHI

 • Mayai ya kuchemsha 2
 • Chungwa 1
 • Green tea kikombe 1

MCHANA

 • Viazi mviringo vya kuchemshwa vinne
 • machungwa 2

USIKU

 • Bakuli kubwa la mboga za majani (Spinach/mchicha/kabichi/majani ya kunde nk)
 • Vipande viwili vya samaki wa kuchemsha

SIKU 3

ASUBUHI

 • Mayai ya kuchemsha 2
 • Chungwa 1
 • Green tea kikombe 1

MCHANA

 • Nyanya 1
 • Viazi vitamu vipande 2
 • chungwa 1

USIKU

 • Bakuli kubwa la salad / kachumbari
 • Mayai ya kuchemshwa 2
 • Chungwa 1

SIKU YA 4

ASUBUHI

 • Mayai ya kuchemsha 2
 • Chungwa 1
 • Green tea kikombe 1

MCHANA

 • Viazi mviringo vya kuchemshwa vinne
 • machungwa 2

USIKU

 • Bakuli kubwa la salad / kachumbari
 • Bakuli dogo la njegere au maharage (Yalioungwa au yasiyoungwa)
 • Tango 1

SIKU YA 5

ASUBUHI

 • Mayai ya kuchemsha 2
 • Chungwa 1
 • Green tea kikombe 1

MCHANA

 • Viazi vitamu vya kuchemshwa vipande 2
 • machungwa 2

USIKU

 • Bakuli kubwa la salad / Kachumbari
 • Kuku 1/4 (au nyama ya aina nyingine)

SIKU YA 6

ASUBUHI

 • Mayai ya kuchemsha 2
 • Chungwa 1
 • Green tea kikombe 1

MCHANA

 • Bakuli ka salad ya matunda mchanganyiko (Mf tikiti maji, matango, apple, mapeaches, berries, embe, parachichi, papai, ndizi nk).

USIKU

 • Bakuli kubwa la salad / Kachumbari
 • Samaki vipande 2 vya kuchemsha , kuchoma au kuoka
 • Chungwa 1

SIKU YA 7

ASUBUHI

 • Mayai ya kuchemsha 2
 • Chungwa 1
 • Green tea kikombe 1

MCHANA

 • Viazi vitamu vya kuchemshwa vipande 2
 • machungwa 2

USIKU

 • Bakuli kubwa la salad / Kachumbari
 • Mayai ya kuchemsha 2

TAHADHARI

Diet ya mayai ni nzuri pale tu unapohitaji kupunguza kiasi kikubwa cha uzito kwa muda mfupi endapo kuna dharura inayokulazimu kupungua.

Kutokana na sababu hii, diet hii si rahisi kuifata kwasababu itakulazimu kula kiasi kidogo sana cha chakula hivyo kukusababisha kuhisi njaa ya mara kwa mara.

Pia haupaswi kuifata diet hii zaidi ya wiki moja kwasababu mwili wako unahitaji virutubisho kutoka kwenye vyakula tofauti tofauti.

Watu wasioruhusiwa kufata diet hii ni wale wenye

 • Ujauzito
 • Wamama wanaonyonyesha
 • Tatizo la cholesterol kuzidi
 • Wenye allergy ya mayai

You may also like...

10 Responses

 1. Lucia Enoq says:

  Diet hii inaweza kusaidia kupunguza kilo ngapi kwa wiki?
  Na pia mtu anaweza kuendelea na hii diet akiwa anafanya mazoezi?
  Asante sana😘

  • GigiMaenda says:

   Uzito unategemeana na uzito wako unaoanzia dear. Kama unaanza na uzito mkubwa basi unaweza kupunguza 3-5 ila kama unaanza na mdogo basi 2-3 kg. Wengi walionipa mrejesho wamepunguza 3 kg na 4 kg.

   Unaweza kufanya mazoezi kama unajisikia mwili wako una nguvu. Kama unaona hauna nguvu unaweza kutofanya tu. Ila ukifanya ndiyo unaongeza uwezekano wa kupunguza uzito mkubwa zaidi!

   Asante sana na wewe kwa kupitia hapa kujifunza dear! Ninatumaini utashirikisha blog hii na ndugu na rafiki zako nao waweze kupata elimu nzuri! Karibu tenaaa!

 2. Sophia Philemon says:

  My dear nmesoma na nmefuatilia kiukweli kwa kusoma tu nmejisikia Faraja sana ila nlikuwa nauliza mtu mwenye vidonda vya tumbo anaruhusiwa kufanya hii diet? Nakuomba sana unisaidie

  • GigiMaenda says:

   Asante sana kwa kuja kujifunza dear, nimefurahi sana kuwa umefurahia makala. Kwa watu wenye vidonda vya tumbo wasiotumia dawa kila siku hii haiwafai dear. Labda kama mtu anatumia dawa na anaweza kuhakikisha kuwa anagawa chakula ili awe anakula kwa muda maalum, au aongeze chakula kidogo katikati ya milo ili tumbo lisiwe wazi kwa muda mrefu!

 3. Diana says:

  Ahsante kwa masomo mazuri, nitafanya hizo diet za dharura na matokeo nitaleta hapa😘

  • GigiMaenda says:

   Asante na wewe kwa kupitia dear😍 Nitafurahi sana kupata matokeo yako!💃🏾💃🏾 Najua yatakuwa mazuri!

 4. Unnie says:

  Samahan dada hivi kati ya supu ya kabichi Na diet ya mayai ni ipi inapunguza kilo haraka?

  • GigiMaenda says:

   Bila samahani dear🤗 Zote zinapunguza around uzito sawa usijali fanya yoyote ambayo unaona mahitaji yake ni rahisi kuyapata!

 5. Amina says:

  Habari Dada naomba kuuliza kwamba maziwa fresh yanawez kutumik badal ya green tea

  • GigiMaenda says:

   Hapana dear, green tea hauwezi kunadilisha na maziwa. Kama utakisa kabisa unaweza kutumia majani ya mchai chai.

   Badala ya kuyachemsha wewe yaloweke kwa dakika 5-10 kwenye maji ya chai yaliyochemka kisha ndio unywe.

COMMENT