DIET YA MATANGO YA KUPUNGUZA UZITO HARAKA

Diet ya matango ni diet fupi ambayo lengo lake ni kukusaidia kupunguza uzito mkubwa ndani ya muda mfupi.

Diet za aina hii hutakiwa kutumiwa kama hatua ya dharura tu na sio ya muda mrefu. Unaweza kufata ratiba hii kwa muda wa kuanzia siku 3 hadi 7 kulingana na uwezo wako.

Kama kutokana na sababu moja au nyingine hautaweza kufanya diet hii wala usiwe na shaka. Zipo diet 4 nyingine za dharura zilizoelezewa kwa kina kwenye blog hii.

Ukiishindwa hii bila shaka utaweza kufanya moja wapo kati ya hizo nyingine.

SOMA: DIET YA KABICHI

SOMA: DIET YA UKWAJU

SOMA: DIET YA MTINDI

SOMA: DIET YA MAYAI

Yaliyomo

 • Kiasi cha kalori kwenye matango
 • Faida za matango
 • Jinsi ya kuanza diet ya matango
 • Vyakula vinavyoruhusiwa
 • Ratiba ya siku 7
 • Tahadhari

KIASI CHA KALORI KWENYE MATANGO

Matango hupatikana katika ukubwa tofauti tofauti.

Kwa hiyo namba unazoenda kuziona ni kiasi kinachopatikana katika tango moja lenye uzito wa gramu 280.

VIRUTUBISHOKIASI
Kalori 42
Protini 1.8 g
Wanga 10 g
Mafuta 0.3 g
Nyuzi nyuzi (Fibre) 1.4 g
Maji 95%

FAIDA ZA MATANGO

1. VITAMIN NA MADINI

Matango yana aina mbali mbali za vitamin na madini muhimu sana kwa afya ya binadamu.

Virutubisho hivi ni kama:

 • Vitamin C (14% ya kiasi kinachohitajika kwa siku)
 • Vitamin K (62% ya kiasi kinachohitajika kwa siku)
 • Magnesium (10% ya kiasi kinachohitajika kwa siku)
 • Potassium (13% ya kiasi kinachohitajika kwa siku)
 • Manganese (12% ya kiasi kinachohitajika kwa siku)

2. MAJI

Kama ulivyoona kwenye jedwali hapo juu, asilimia 95% ya matango ni maji. ( 1 )

Maji ni muhimu sana kwa viumbe hai, faida zake ni nyingi sana nikiziandika zote makala hii itakuwa ndefu sana!

Baadhi ya faida muhimu muhimu kuliko zote za maji ni kusaidia kuweka joto la mwili sawa kwa njia ya kutoka jasho.

Pamoja na kusaidia usafirishaji wa virutubisho kwenda kwenye seli za mwili, na utoaji wa takamwili kutoka kwenye hizo seli na kuzitoa nje ya mwili.( 2 )

Tafiti nyingi za kisayansi zimeonesha kuwa watu wenye mazoea ya kunywa maji mengi hupunguza uzito kwa ufanisi zaidi kuliko wale wasiopenda kunywa maji.

Kwa hiyo matango ni mazuri sana hasa kwa wale watu ambao huwa hawawezi au hawapendi kunywa maji.

PUNGUZA UZITO KWA KULA MATANGO

3. KALORI CHACHE

Matango yana kiasi kidogo cha kalori ukilinganisha na matunda mengine mengi.

Hii ni kwasababu asilimia 95 ya tunda hili ni maji. Pia ni kwasababu matango yana kiasi kidogo sana cha mafuta na sukari.

Kutokana na hili unaweza kula matango mengi na kupata virutubisho vingi bila kupitiliza kimo chako cha kalories cha siku.

4. KUSHUSHA SUKARI

Tafiti nyingi za kisayansi zimeonesha kuwa matango husaidia kucontrol sukari kwenye damu. ( 3 )

Lakini kwa sasa tafiti hizi zimekuwa zikifanyika katika wanyama tu na si kwa binadamu.

Kwahiyo bado haijajulikana ni kiasi gani au ni kwa njia gani inaweza kuleta matokeo kama haya kwetu.

5. KUPATA CHOO LAINI

Sababu kuu mbili za tatizo la kupata choo ngumu (Constipation) ni upungufu wa maji na nyuzinyuzi. ( 4 )

Hasa kwa wale watu ambao husahau kunywa maji, matango husaidia sana katika kuhakikisha unapata choo kwa kawaida.

6. KUPUNGUZA UZITO

Matango husaidia kupunguza uzito kutokana na faiza zote zilizotajwa hapo juu.

Unapokuwa katika harakati za kupunguza uzito mara nyingi utajikuta ukihisi njaa mara kwa mara.

Hii ni kwasababu kwa kawaida tunahitaji kupunguza kiasi chetu cha chakula ili kufanya miili yetu itumie mafuta tuliyonayo na kuyageuza nguvu.

Matango ni mazuri kutumia kama nyenzo ya kuzuia njaa. Hii ni kwasababu yana maji mengi na nyuzi nyuzi ambazo hukufanya ushibe kwa muda mrefu zaidi na hivyo kukuzuia kula mara kwa mara.

JINSI YA KUFATA DIET YA MATANGO KWA AJILI YA KUPUNGUZA UZITO HARAKA.

Kwanza kabisa nikukumbushe tena kuwa hii ni diet ya dharura inayotakiwa kufatwa kwa muda wa siku 3-5 tu.

Diet zote za dharura zina kikomo kwasababu huwa zinalazimu mtu kula kiasi kidogo sana cha chakula (kalori) ili kupunguza uzito haraka.

Zipo aina nyingine za diet ya matango ambazo zinalazimisha mtu kula matango tu kwa hizo siku zote 7.

Lakini kutokana na kufata misingi ya afya nimechagua ile diet isiyokuwa na sheria kali sana na kuongeza vitu muhimu.

Lengo la kufanya hivi ni kuhakikisha unakuwa na nguvu za kutosha na unafurahia vyakula aina nyingine badala ya matango tu.

VYAKULA VINAVYORUHUSIWA

PROTINI: Nyama, samaki, mayai, mtindi, jamii ya kunde.

WANGA : Wali wa brown, mkate wa brown

MBOGA MBOGA: Mboga za majani, Nyanya, Kitunguu, Zuccini. pilipili hoho, Celery, Kabichi, Karoti.

MATUNDA: Matango, Apple.

SMOOTHIE YA TANGO

DIET YA SIKU 7
 • Tango kubwa 1
 • Apple 1
 • Celery kipande kimoja
 • Spinach changa (baby spinach)

Vuruga mahitaji yote kwenye blender

RATIBA YA SIKU

SIKU YA 1

ASUBUHI

 • Mayai ya kuchemsha 2
 • Tango 1
 • Green tea au kahawa

MCHANA

 • Tango kubwa 1
 • Kuku 1/4 (au nyama ya aina nyingine)
 • Maziwa ya mtindi Robo Lita

USIKU

 • Tango kubwa 1
 • Wali wa brown Vijiko vikubwa 16
 • Mboga za majani

SIKU YA 2

ASUBUHI

 • Mayai ya kuchemsha 2
 • Tango 1
 • Green tea au kahawa

MCHANA

 • Matango mawili
 • Kachumbari
 • Mtindi plain (usioongezwa ladha au sukari kiwandani) robo Lita

USIKU

 • Mkate wa brown slesi 2
 • Maharage bakuli ndogo 1
 • Salad ya tango 1

SIKU 3

ASUBUHI

 • Tango kubwa 1
 • Apple 1
 • Green tea kikombe kimoja

MCHANA

 • Wali wa brown vijiko vikubwa 16
 • Samaki vipande viwili (Chemsha/choma/oka)
 • Mboga za majani
 • Tango kubwa 1

USIKU

 • Salad ya matango (Bakuli kubwa 1)
 • Karanga kiganja kidogo 1

SIKU YA 4

ASUBUHI

 • Smoothie ya tango
 • Mayai ya kuchemsha 2

MCHANA

 • Tango kubwa 1
 • Kuku 1/4 au nyama ya aina nyingine
 • Kachumbari bakuli 1

USIKU

 • Tango kubwa 1
 • Bakuli dogo la njegere au maharage (Yalioungwa au yasiyoungwa)
 • Mkate wa brown slesi 2

SIKU YA 5

ASUBUHI

 • Smoothie ya tango
 • Mayai ya kuchemsha 2

MCHANA

 • Matango mawili
 • Kachumbari
 • Mtindi plain robo Lita

USIKU

 • Wali wa brown vijiko vikubwa 16
 • Samaki vipande viwili (Chemsha/choma/oka)
 • Mboga za majani
 • Tango kubwa 1

SIKU YA 6

ASUBUHI

 • Tango kubwa 1
 • Apple 1
 • Maziwa ya mtindi plain robo lita

MCHANA

 • Salad ya matango (Bakuli kubwa 1)
 • Karanga kiganja kidogo 1

USIKU

 • Tango kubwa 1
 • Bakuli dogo la njegere au maharage (Yalioungwa au yasiyoungwa)
 • Mkate wa brown slesi 2

SIKU YA 7

ASUBUHI

 • Tango kubwa 1
 • Apple 1
 • Maziwa ya mtindi robo lita

MCHANA

 • Wali wa brown vijiko vikubwa 16
 • Samaki/nyama/ (Chemsha/choma/oka)
 • Mboga za majani
 • Tango kubwa 1

USIKU

 • Tango kubwa 1
 • Bakuli kubwa la salad
 • Mayai ya kuchemsha 2
DIET YA KUPUNGUZA TUMBO

TAHADHARI

Diet ya matango ni nzuri pale tu ambapo una dharura na unahitaji kupunguza uzito mkubwa kwa muda mfupi.

Haupaswi kuifata diet hii zaidi ya wiki moja wala haupaswi kuirudia rudia mara kwa mara ndani ya muda mfupi.

Upo uwezekano mkubwa sana wa kurudisha uzito wote uliopunguza katika diet hii. Hii itatokea endapo utarudi tena kwenye kula kiasi kikubwa cha vile vyakula vilivyokusababisha kuongezeka uzito.

Watu wasioruhusiwa kufata diet hii ni wale wafuatao.

 • Wamama wajawazito
 • Wamama wanaonyonyesha

KWA KIFUPI

Diet ya matango ni diet fupi ambayo inaweza kukusaidia kupunguza uzito mkubwa pale unapokuwa na dharura.

Ili kupata mafanikio ya kudumu katika safari yako ya kupunguza uzito inashauriwa kujifunza misingi ya lishe bora ili uweze kupata matokeo ya kudumu.

Kwa hiyo kumbuka kuendelea kula kiasi na aina sahihi ya vyakula mara baada ya kumaliza diet yako ya dharura.

Zipo makala nyingi sana kwenye blog hii zitakazokuelekeza jinsi ya kuanza safari ya kudumu ya kupunguza uzito na kuishi kwa afya.

Kwa hiyo nitafurahi kama utaendelea kusoma huku ukiendelea kufata hii diet ya dharura.

You may also like...

6 Responses

 1. Moyo says:

  Hapa kwnye karanga sijaelewa mpnz ni karanga kavu?

  • GigiMaenda says:

   Karanga zozote dear, mbichi au za kupikwa!

  • nickson clinton says:

   daaah sasa, ungetuandikia matokeo yatokanayo na diet hii i mean side effect maana leo nina siku ya tatu but jana nimeanza kuharisha maji yenye mbegu za matango je hakuna madhara

   • GigiMaenda says:

    Oh pole sana! Katika research na experience za watu sijawahi kusikia mtu kapata kuharisha kutokana na hii diet. Lakini mwisho wa siku binadamu tuna miili tofauti kwa hiyo labda wewe inakupa shida.

    Mara nyingi kuharisha husababishwa na bacteria au virus ambao unawe za kupata katika chakula ambacho hakiajaoshwa au kupikwa ipasavyo. Mbegu za matango kwenye choo ni kawaida usihofu hilo.

    Je umeharisha mara ngapi kwa siku? na kwa siku ngapi hadi sasa. Kama inafika mara 5-10 kwa siku na unahisi ni sababu ya diet basi acha kwaanza diet na uendelee kula vyakula vinavyosaidia kupunguza kuharisha kama Viazi, ndizi, uji wa mchele,mkate au supu isiyoungwa ili kusaidia kuzuia kuharisha na kuzuia kupungua maji mwilini.

    Kwa kawaida kuharisha huwa kunaacha kwenyewe lakini kama kutaendana na dalili zifuatazo ni vizuri kwenda hosptali
    1.Kuharisha zaidi ya siku 3
    2.Maumivu makali sana ya tumbo
    3.Damu kwenye choo kubwa au choo kubwa cheusi
    4.Homa
    5.Kuishiwa nguvu sana
    6. Kiu kali sana
    7. Kukauka mdomo
    8. Kupungua au kukosa haja ndogo

    Jifuatilie leo kwa makini, fuatilia umepata choo ya maji mara ngapi halafu nitafurahi kama utanipa mrejesho kuhusu hali yako inavyoendelea.

 2. Jasmine says:

  Habari na je uliwa unakula matango peke yake bill kula kitu kingine

  • GigiMaenda says:

   Salama dear, ukifanya hivyo utahisi njaa sana na unaweza kupata hata kizunguzungu maana chakula kitakuwa kidogo sana.

COMMENT