DIET YA SUPU YA KABICHI YA KUPUNGUZA UZITO!

Diet ya supu ya kabichi ni aina ya diet ambayo imeundwa kwa ajili ya kusaidia kupunguza uzito kwa muda mfupi wa siku 7.

Zipo diet nyingine za muda mfupi ambazo zimeandikwa kwenye blog hii kama zifuatavyo.

SOMA: DIET YA JUISI YA UKWAJU

SOMA: DIET YA MTINDI

SOMA: DIET YA MAYAI

Hii ni diet ya kufatwa kwa siku 7 na kila siku ina mwongozo wake wa jinsi ya kula.

Chakula kikubwa unachotakiwa kula kwa wingi kila na kwa kiasi chochote unachohitaji ni supu ya Kabichi.

Kila siku utakuwa unakula hii supu pamoja na vyakula vingine utakavyoviona hivi punde.

VYAKULA VYA WIKI MOJA TU KWA KUPUNGUZA UZITO/TUMBO HARAKA!

MAHITAJI YA KUTENGENEZA SUPU YA KABICHI:

 • Kabichi 1
 • vitunguu 6
 • Pili pili hoho 2 (Nyekundu/njano/kijani)
 • Carrots 3
 • Vitunguu vya majani (green onions/scallions) fungu 1
 • Celery fungu 1
 • Nyanya kubwa 6
 • Limao
 • Vitunguu saumu
 • Maji /soup ya kuku/ soup ya mboga mboga

HATUA:

 • Tumia vijiko vichache vya mafuta ya kupikia kukaanga vitunguu, hoho,Karoti,celery, vitunguu saumu na kabichi.
 • Zikiwa tayari weka nyanya, chumvi na viungo vingine unavyopendelea kama cumin, black pepper nk.
 • Weka maji/chicken stock/vegetabe stock kisha punguza moto na ufunike chakula kiive kwa saa 1-2.

SIKU YA 1: MATUNDA

Siku hii kula supu ya kabichi yako kiasi chochote unachohitaji pamoja na matunda yoyote kasoro NDIZI.

Kunywa maji kwa wingi, chai labda isiwe na sukari kama una mbadala wa sukari ( sweetners zipo za aina nyingi).

SIKU YA 2: MBOGA MBOGA

diet ya supu ya kabichi inavyopunguza mwili haraka

Kula mboga mboga kama karoti, zuccini, nyanya, mboga za majani kiasi unachohitaji bila kusahau supu ya kabichi kila unapohisi njaa.

Ongeza kiazi mviringo cha kuchemsha au kuoka kimoja kwenye mlo wako wa jioni.

SIKU YA 3: MATUNDA NA MBOGA MBOGA

Kula supu yako pamoja na matunda na mboga mboga kama siku ya kwanza na pili.

Kumbuka kuepuka ndizi na kula kwa kiasi kama matunda yako yana sukari nyingi sana.

SIKU YA 4: MAZIWA SKIMMED NA NDIZI

Unaruhusiwa kula ndizi siku hii. Unaweza kula ndizi hadi 8 pamoja na maziwa ya skimmed.

Unaweza kutengeneza smoothie au milkshake ya ndizi na maziwa ambayo ni skimmed.

Kama kawaida usisahau kula supu ya kabichi yako unapohisi njaa.

SIKU YA 5: NYAMA YA NG’OMBE NA NYANYA

Kula nyanya ndogo 6 au kubwa 3 pamoja na supu ya kabichi.

Unaweza kukata kama kachumbari ukaweka na kitunguu au ukala kawaida.

Pia unaruhusiwa kula 1/4 kg hadi 1/2 kilo ya nyama ya ng’ombe ya kuchemsha au kuchoma.

Kama hauna/hautumii/haupendelei ya ng’ombe tumia kiasi hicho hicho cha nyama ya kuku bila ngozi.

SIKU YA 6: NYAMA NA MBOGA MBOGA

Kula supu ya kabichi angalau mara moja siku hii huku ukila nyama/samaki/kuku na mboga za maji kwa kiasi unachohitaji.

SIKU YA 7: WALI, MBOGA MBOGA NA JUICE

Pamoja na supu yako siku hii ya mwisho unaruhusiwa kula brown rice.

Pia kunywa juisi ya matunda ambayo haijaongezewa sukari.

Diet hii inafanya ule kiasi kidogo cha chakula au kiasi kidogo cha calories kwa siku kwa hiyo ni muhimu kupata ushauri wa daktari kabla haujaanza.

Kumbuka usitumie hii diet ya supu ya kabichi kama mbinu ya kudumu ya kupunguza uzito wa mwili wako.

SOMA: NJIA 10 ZA KUPUNGUZA UZITO BILA DIET WALA MAZOEZI

Hii ni njia ya muda mfupi tu kwa ajili ya kupunguza uzito au kupunguza tumbo ili nguo yako ikukae vizuri kama una tukio au shughuli ya kwenda!.

Pia hautakiwi kufata diet ya supu ya kabichi kwa zaidi ya siku saba.

Kama unapendelea kuendelea kupunguza uzito wa mwili wako basi endelea na kula vyakula sahihi au fata diet ya kupunguza uzito ya muda mrefu.

KWA KIFUPI NI HIVI!

Diet ya supu ya kabichi ni nzuri kwa kupunguza uzito haraka kwa ajili ya shughuli fulani, sio kwa ajili ya matokeo ya kudumu, asilimia kubwa uzito uliopungua utarudi utakaporudi kula vyakula vyako vya kawaida.

Itumie ipasavyo, pata matokeo halafu endelea na healthy lifestyle ili upunguze uzito wa mwili kwa muda mrefu.

Kama umewahi kufata diet hii tafadhali tushirikishe matokeo yako na kama haujawahi ila utajaribu baada ya kujifunza leo basi usisahau kutupa feedback ya matokeo yako.

SOMA: VYAKULA VYA ASUBUHI (VIFUNGUA KINYWA) VINAVYOSAIDIA KUPUNGUZA UZITO HARAKA

You may also like...

2 Responses

 1. Monica says:

  Nimependa sana mwongozo wako mpendwa natumaini tutakuwa pamoja

COMMENT