AINA KUU ZA DIET ZA KUPUNGUZA UZITO.

Baada ya kufanya maamuzi ya kupunguza uzito wa mwili wako ni muhimu sana kufanya uchunguzi na kuchagua kufuatilia aina gani ya mfumo wa kula chakula kwa ajili ya kupungua(DIET)

Zipo aina nyingi na mara nyingi watu hawazijui hivyo wanafanya makosa mengi yanayowafanya uzito wanaopunguza kurudi tena na tena.

Kwenye kipengele hiki ninaelezea Diet kubwa zinazotambulika na kufatwa na watu wengi zaidi duniani na zenye mafanikio makubwa sana katika kupunguza uzito!

1. KUPUNGUZA KIASI CHA CHAKULA:

getty_rf_photo_of_three_different_portions_0

Hii inajieleza yenyewe, kila mtu anajua kula chakula kingi sana kunasababisha kuongezeka uzito, hivyo ukitaka kupungua kwanza anza kwa kupunguza kiasi cha chakula unachokula wakati huu, badala ya chai na chapati tatu kula mbili, badala ya wali sahani mbili kula moja, au badala ya soda 4 kwa siku punguza unywe moja.

Mtu yeyote ambaye ndiyo kwanza ameanza mikakati ya kupunguza uzito wa mwili anashauriwa kuanza na njia hii, halafu baada ya kuzoea kula chakula kiasi kinachotakiwa ndiyo unaweza kuongeza jitihada nyingine za kupungua.

UZURI: Njia hii haikuzuii kula vyakula unavyovipenda ukilinganisha na diet nyingine ambazo huwa zinazuia au zinakulazimu upunguze aina Fulani ya vyakula.

UGUMU: Unaweza kusikia kama haushibi au njaa mara kwa mara kwasababu tumbo lako linakuwa lilizoea kuwa cha chakula kingi sana. Hii huacha baada ya muda na ita kuwa kawaida.

2. KUPUNGUZA MAFUTA (LOW FAT DIETS):

pepper-pork-vegetable-and-basil-stir-fry-88576-1

Mara nyingi aina njia hii inakulazimu ule vyakula vya protein kwa wingi kwasababu vyakula vya protein vinashibisha sana na ndivyo malighafi inayotumika kutengeneza misuli.

Pia unashauriwa kula nafaka zisizokobolewa kama UNGA WA DONA badala ya mweupe, BROWN BREAD, BROWN RICE, BROWN PASTA n.k pamoja na Viazi vitamu badala ya mviringo, ndizi mbichi, oats n.k

Ili kuepuka kutumia kiasi kikubwa cha mafuta, KUCHEMSHA, KUOKA na KUCHOMA ndiyo njia maalumu zinazotumika kupika chakula katika aina hii ya diet.

Mafuta unatumia lakini kwa kiasi kidogo, na inashauriwa kutegemea mafuta ya matunda kama PARACHICHI na karanga kuliko mafuta ya kwenye nyama na ya kupikia.

UZURI: Kila mtu anapenda vyakula vya wanga, vinapatikana kwa bei nzuri, unaweza kula matunda ya aina mbalimbali.

UGUMU: kuzoea vyakula visivyokaangwa, kuzoea kula nafaka zisizokobolewa kama dona, brown rice, brown bread, brown pasta.

3. KUPUNGUZA VYAKULA VYA WANGA (LOW CARB DIETS):

Zipo aina kuu mbili za DIET hii, ya kwanza ya kupunguza wanga, kuongeza mafuta na protein kiasi (LOW CARBOHYDRATE, MODERATE PROTEIN, HIGH FAT) hii inaitwa KETOGENIC DIET, na ya pili ni ya kupunguza wanga, kuongeza protein na mafuta kiasi (LOW CARB, HIGH PROTEIN, MODERATE FAT).

Katika aina hii ya diet hautakiwi kula kula vyakula vya wanga kama ugali, wali, viazi pamoja na aina nyingi za matunda kwa sababu matunda mengi huwa na sukari nyingi sana.

Wanga utapata kutoka kwenye mboga mboga, maziwa na aina mbalimbali za karanga kasoro korosho kwasababu nazo zina sukari nyingi sana.

low-carb-guide-2-1-800x392

Kwasababu huli vyakula vya wanga mwili wako utaanza kuyeyusha mafuta yaliyo tayari mwilini ili kutengeneza nguvu kwa ajili ya shuguli mbali mbali.

UZURI: Unaweza kula vyakula vya kukaanga, jibini (cheese), nyama kwa wingi sana, karanga na uzito unapungua haraka zaidi.

UGUMU: Kuacha kula vyakula vya wanga ni shughuli kwasababu miili yetu imezoea kutumia vyakula vya wanga kutengeneza nguvu. Fikiria kula mboga tupu bila ugali au wali, au viazi etc.

Pia unahitaji kuwa makini sana kuhakikisha huzidi kiasi kima cha mwisho cha kiasi cha vyakula vya wanga, inamaana lazima upime vyakula unavyokula ili uwe sahihi.

4. KUTOKULA WANYAMA NA VITU VINAVYOTOKANA NA WANYAMA( VEGETARIAN/VEGAN DIET):

vegan

Vegetarians hawali nyama ila wanakula vitu vinavyotokana na wanyama kama maziwa, mayai, jibini (cheese) mayonnaise n.k, wengine wanakula samaki (pescatarian) ila wengine hawali.

Vegans hawali wanyama wala kitu chochote kinachotokana na wanyama, wanakula mimea tu.

Duniani watu wengi wanaokula hivi wanakuwa na afya nzuri sana hasa vegans, nadhani umewahi kusikia kuwa Rastafarians wale wa ukweli huwa hawanenepi wala hawaumwi mara kwa mara kutokana na kufata aina hii ya diet.

Mimea ina virutubisho vingi sana na haina cholesterol kama nyama, kwa hiyo mfumo huu wa ulaji huzuia magonjwa mengi sana ambayo husababishwa na kula wanyama.

UZURI: Utajisikia wa afya sana, kama una magonjwa kama gout, chunusi za kupitiliza, kuumwa sana wakati wa period kwa wanawake n.k vitapungua sana!

UGUMU: Kuacha kula nyama, mayai, maziwa ni ngumu sana kwa watu wengi.

Watu wengi duniani hutumia njia hizo kupunguza uzito wa mwili na kurejesha afya ,unapochagua njia ipi inakufaa unapaswa kufahamu kuwa diet hizi siyo za kufanya kwa muda mfupi halafu urejee kwenye ulaji wa mwanzo.

Ni muhimu kuamua kufanya mabadiliko ya muda mrefu ili uweze kupunguza uzito na kuwa na afya kwa muda mrefu pia.

Je kati ya diet hizo ipi unaona utaimudu kwa muda mrefu?

You may also like...

COMMENT